Thursday, June 22, 2017

WAKAZI WA CHANG'OMBE JIJINI DAR ES SALAAM WAZAWADIWA MRADI WA MAJI WENYE THAMANI YA SH. MILIONI 68

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia), akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa Chang'ombe B, Mgeni Hamisi Ramadhani wakati wa uzinduzi mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Meneja Miradi Endelevu wa SBL, Hawa Ladha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Helene Weesie (kulia) na Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo.
Diwani wa Kata ya Chang'ombe, Benjamini Ndalichako , akisoma hutuba kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Temeke ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye hafla hiyo. Kulia ni Diwani wa Viti Maalumu, Mwanakombo Mwinyimvua na kushoto ni Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa katika eneo hilo.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, John Wanyanja akizungumza kwenye hafla hiyo kuhusu mradi huo.
Uzinduzi ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale

KAMPUNI ya Bia Serengeti leo imezindua mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni 68 uliopo katika eneo la Chang’ombe ‘B’ wilayani Temeke, jijini Dar es Salaam ikiwa ni jitihada za kuwaletea maji safi na salama wakazi wa eneo hilo.

Ukiwa na uwezo kwa kuhudumia watu 4,000 mradi huo unajumuisha kisima pamoja na mifumo yake, pampu ya maji inayotumia nishati ya jua na tenki la maji ambapo zinazalishwa lita 20,000 za maji kwa kila masaa ishirini na nne.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Helene Weesie alisema kuwa mradi huo ambao unajulikana, “Maji kwa Uhai” ni miongoni mwa mikakati kama hiyo ambayo kampuni ya bia imeiendesha katika mikoa ya Iringa, Kilimanjaro, Mwanza, Tanga, Ruvuma, Dar es Salaam, Pwani na Dodoma ikiwa inawanufaisha zaidi ya watu milioni moja kwa maji safi na salama.

Weesie alisema kwamba mradi wa Chang’ombe sio tu kwamba utaboresha afya za wakazi wa eneo hilo bali pia utaongeza tija kiuchumi, “hususani kwa watoto wa kike na wanawake ambao hawatahitaji kutumia saa nyingi kutafuta maji safi sehemu nyingine. Hii inawapa fursa ya kuhudhuria shule wakiwa huru.”

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu