Friday, June 23, 2017

WAZIRI KAIRUKI AFUNGUA SEMINA YA TAKWIMU HURIA KWA WADAU JIJINI DAR ES SALAAM

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora , Angela Kairuki akizungumza na wadau wa Takwimu wakati wa Semina ya upatikanaji wa Takwimu huria katika ofisi za Serikali iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama , ambapo wadau wa takwimu walijadili umuhimu wa Takwimu Huria ili kuwawezesha wananchi kupanga maendeleo yaokulingana na takwimu halisi.
Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa Semina ya Takwimu huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama jijini Dar es Salaam ambapo wadau wa Takwimu walipata kujadili umuhimu wa upatikanaji wa Takwimu huria katika ngazi mbalimbali.
Mkurugenzi wa Usimamizi wa huduma za Umma na Utendaji kutoka Benki ya Dunia nchini, Jim Brumby akizungumza na wadau wa takwimu juu ya umuhimu wa upatikanaji wa takwimu huria katika kupanga mipango ya maendeleo.
Mkurugenzi wa shughuli za kitakwimu nchini kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu a,Irenius Ruyobya akitoa neno la shukrani kwa wadau waliofika katika semina ya Takwimu huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau kutoka sekta za serikali na binafsi walioshiriki katika Semina hiyo
Mtaalamu mkuu wa Utawala kutoka Benki ya Dunia Tanzania , Verena Luise akizungumza wakati wa Semina hiyo kwa wadau wa Takwimu huria iliyofanyika katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Twaweza nchini, Aidan Eyakuze akionyesha ni jinsi gani watanzania wachache waliotembelea Takwimu huria na nini kinahitajika hili kila mtu aweze kuzifikia hizo Takwimu.
Mshauri Mwelekezi wa Takwimu huria, Rose Aiko akizungumza juu ya umuhimu wa Takwimu huria kwa wadau walioshiriki semina hiyo katika ukumbi wa COSTECH Kijitonyama.
Sehemu ya Washiriki wa semina ya Takwimu huru wakiwa wanasikiliza kwa Makini.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu