Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ,akizungumza wakati wa Swala ya Idd el Fitry iliyofanyika kitaifa katika Msikiti wa Riadha mjini Moshi.
Mufti wa Tanzania na Sheakh Mkuu, Abubakary Bin Zubery akitoa nasaha zake wakati wa Swala ya Idd iliyofanyika kitaifa mjini Moshi.
Waumini wa Dini ya Kiislamu wakishiriki katika Swala ya Idd El Fitry iliyofanyika mskiti wa Riadha mjini Moshi

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii ,Kanda ya Kaskazini.

SERIKALI imeahidi kuongeza kasi katika zoezi la ukamataji wa wahusika wa matukio ya mauaji yaliyotokea Kibiti,Rufiji na Mkuranga mkoani Pwani na kuhakiksha wanafikishwa mbele ya vyombo vya sharia.

Waziri Mkuu wa Tanzania ,Kassim Majaliwa aliyasema hayo jana katika baraza la Idd lililofanyika kitaifa katika mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro lkitanguliwa na Swala ya Idd El Fitri iliyofanyika kitaifa katika msikiti wa Riadha.

“Kinachofanyika sasa nikuhakikisha kwanza tunawapata waharifu halisi ilikuepuka kuingiza watu wasio husika, kama vile hao wenye hisia kwamba mauaji haya yanafanywa labda na waislamu hapana .”alisema Mh Majaliwa .

Alisemakaz kubwa inayofanywa sasa ni kuchuja na kujua nani hasa anshiriki katika mauaji hayo huku akiwashukuru watanzania ambao tayari wameanza kutoa ushirikiano kwa kuanza kueleza nani wanahusika katika tukio hilo.

“Kazi yetu ni kuwapeleleza pale ambapo tunauthibitisho wa ushiriki wao na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao na kazi hiyo inaendelea vizuri.”alisema Majaliwa.

Mapema katika taarifa ya Baraza kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) iliyosomwa na kaimu katibu Mkuu,Sheakh Salim Amir Abeid alisema Bakwata imeshtushwa na matukio ya mauaji ya kutisha ya watu wasio na hatia katika maeneo ya mkoa wa Pwani.id.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: