Mkuu wa Wilaya Sikonge akifungua Maafunzo ya Maafisa Ugani.
Katibu wa CCM wilaya ya sikonge Emanuel Alex.
Maafisa Ugani wa sikonge wakiwa katika mafunzo.

Wataalamu wa kilimo wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora wametakiwa kuandaa mashamba mapema na kujua mahitaji yao muhimu katika maadalizi hayo ili kupata pembejeo za kilimo mapema na kwa wakati Muafaka kabla ya Msimu wa kilimo haujaisha.

Hayo alibainisha Mkuu wa wilaya ya Sikonge Peres Magiri wakati akifungua Mafunzo Maalumu ya Maafisa ugani katika wilaya yake yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi (COSTECH) kupitia Jukwaa la baiteknolojia nchini (OFAB) yenye lengo la kuwakumbusha na kwenda sambamba na kilimo cha kisasa.

“Tunataka kujua mahitaji mapema na kupeleka mahali ambapo yanahusika ambapo ni serikalini tupate pembejeo kwa wakati kwani zinakuja zinachelewa sas zinawasaidia nini wakulima wetu” alisema Peres.

“Mwaka jana pembejeo za ruzuku zingine tulikataa tu tulisema hatuhitaji ilikuwa nadhani mbegu za mahindi na mpunga tulisema Msimu umeshapita sasa zinakuja za nini lakini kama tutakuwa na maandalizi mapema ili pembejeo zije kwa wakati na wakulima kunufaika na hizo ruzuku naamini”Aliongezea Peres

Aidha kwa Upande mwingine Mheshimiwa Peres aliwataka maafisa hao ugani kuungana na wananchi katika kuwasaidia kuweka chakula cha akiba na cha kutosha ili kuepukana na baa la njaa kwani kwa sasa wakulima hao wamekuwa wakiuza chakula chao huku bado wakiwa hawana ziada ya kutosha.

“Hali ya mvua kwa mwaka huu haikuwa nzuri ila katika wilaya yangu tulipata mvua za kutosha na wakulima wetu wamelima na tunachakula cha kutosha ila kwa kuwa sehemu nyingine hawakupata mvua hivyo nawasihi wakulima kuangalia wasiuze chakula chote bali wawe na akiba ambayo itaweza kuwafikisha hadi katika msimu mwingine wa mavuno”Alisema Peres.

Hata hivyo Katibu wa Chama cha Mapinduzi katika Wilaya Hiyo Emanuel Alex alitoa msisitizo kwa Maafisa hao ugani kutumia elimu waliyopata ili kuanza kulima kilimo cha kisasa ambacho kitaweza kuinua pato lao Zaidi.

“Kwa warsha hii na sisi kama viongozi na maafisa waliohudhuria hapa inatakiwa kutoka na mafunzo haya na kwenda kuyafanyia kazi ili kuanza kuzalisha mazao yetu kwa wingi huku tukiwa tunaenda sambamba na kilimo cha kisasa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: