Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa akifungua Mafunzo ya Maafisa Ugani.
Picha ya Pamoja kati ya Viongozi wa Wilaya ya Urambo,Watafiti pamoja na Maafisa ugani wa Wilaya hiyo.

 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Urambo Magret Nakaingwa

Mkuu wa Wilaya ya Urambo Angelina Kwingwa amewaomba watafiti wa kilimo toka Tume ya Taifa ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) pamoja na Kituo cha Utafiti Ukiriguru wawape elimu nzuri ya kutosha katika kilimo cha Zao la Pamba Maafisa Ugani wa wilaya yake ili waweze kulima kilimo hicho na kiwe chenye tija kwao.

Hayo alibainisha leo katika Ufunguzi wa Mafunzo ya Maafisa hao ugani wapatao 30 katika wilaya ya Urambo,Mafunzo yaliyolenga kukumbushana namna ya kulima kilimo cha kisasa na chenye tija kwa Jamii ya sasa.

Mheshimiwa Angelina aliendelea kwa kusema kuwa katika wilaya yake wanazao kubwa la Tumbaku lakini bado wanahitaji kuwa na zao la pamba ambalo wao wanaona linamanufaa kwao pia.

“Watafiti tunaomba mkatusaidia katika mafunzo yenu kufundisha hawa maafisa ugani kulima zao hilo la pamba,japo wao wanalima lakini bado hatujafanya vizuri hivyo tunahitaji maafisa hao wapate mafunzo katika zao hili ili tuanze kulima na tukafanikiwa kama wilaya nyingine”Alisema Angelina.

Aidha Mkuu huyo wa Wilaya aliongezea kwa kuwaomba Maafisa hao ugani kuchukua mafunzo hayo na kwenda kufanyia kazi katika sehemu zao husika ili yaweze kuzaa matunda kwao na kuboresha mazao ambayo wanalima sasa.

‘Lakini pia niwaombe maafisa ugani kuchukua fursa hii na kuelewa unakwenda kupambana vipi katika kituo chako cha kazi ili kuanza kuleta mafaniko katika wilaya yetu na kuanza kuwa na kilimo cha kisasa,Na kama tusipoona matokeo najua wewe ndo utakuwa na matatizo na si wakulima”Aliongezea Angelina.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Urambo Magret Nakaingwa alibainisha kuwa Ulimaji wa zao moja kama vile wao wanavyotegemea Tumbaku kumepelekea wakulima wengi kukosa namna ya kujikimu kimaisha kutokana na soko la Tumbaku kushuka kwa kasi.

“Uchumi wa wilaya ya Urambo unategemea zaidi zao la Tumbaku na msimu huu wa Mavuno changamoto ambayo wakulima wamekutanayo ni kwamba masoko yameenda polepole kwanza yamechelewa kuanza lakini hadi sasa wakulima wanatumbuka katika maghala hawajauza yote”Alisema Magret

“Na kutokana na hilo wakulima wengi wamekosa fedha ambapo imewaathiri sana na sasa wanataka wakulima hao kujikita katika mazao mengine ya biashara ili waweze kuwa na njia nyingine ya kipato”Aliendelea Magret.

Hata hivyo Tume ya Taifa ya sayansi (costech ) kupitia Jukwaa la baiteknolojia nchini (OFAB)imesema itaendelea kutoa Mafunzo kwa Maafisa Ugani katika Wilaya na Mikoa mbalimbali lengo ni kufanya kilimo kiwe cha kisasa ili kufikia azma ya serikali ya awamu ya Tano ifikapo 2025 kuwa Tanzania ya Viwanda.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: