Daktari bingwa wa mifupa na upasuaji wa magoti ambaye pia ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Shalby kutoka nchini India, Dk Vikram Shah akifurahia jambo na Makamu Mwenyekiti wa CCM-Bara, Phili Mangula (katikati) pamoja na Dk Edmund Mndolwa (kushoto) katika halfa ya kusherekea miaka 15 ya huduma za hospitali hiyo barani Africa iliyofanyika jijini Dar es Salaam, hivi karibuni

Dk Vikram Shah akitoa hotuba kwa wageni waliohudhuria halfa hiyo
Baadhi ya wshiriki waliohudhuria hafla hiyo picha na Emmauel Massaka,Globu ya Jamii.
---
Hospitali ya nchini India ya Shalby imeahidi imesherekea miaka 15 ya huduma mbalimbali wanazozitoa za kiafya Afrika huku wakiahidi kuendeleza mashirikiano ili kuboresha afya za Watanzania.

Hayo yamesemwa na daktari bingwa wa mifupa na upasuaji wa magoti kutoka India ambaye pia ni Mwenyekiti na Mkurugenzi Mkuu wa hospitali ya Shalby , Dk Vikram Shah wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Dk Shah amesema timu ya madaktari bingwa kutoka katika hospitali imekuwa ikija Afrika na kufanya kambi za upasuaji mbalimbali ikiwapo upasuaji wa magoti na nyonga.

Amesifu ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na India na kusisitiza kuendelea kusaidiana katika shughuli zao ili kuboresha afya na maisha ya wananchi wa pande zote mbili.

“Tanzania na India zimekuwa na uhusiano wa muda mrefu na kambi za kimatibabu mbalimbali zinazofanywa na madktari wa Shalby nchini na Afrika kwa ujumla ni kithibitisho cha utu na upendo baina ya India na Tanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema Dk Shah.

Dk Shah ambaye anaaminika kuwa daktari aliefanya upasuaji wa kubadilisha magoti mara nyingi zaidi, ambapo mpaka sasa ashafanya upasuaji zaidi ya 85,000, alisema teknolojia ina mchango mkubwa katika kuboresha huduma za afya na kuahidi kuboresha zaidi mashirikiano na Tanzania.

Kwa upande wake daktari bingwa wa mifupa kutoka hospitali ya TMJ, Dk Sylvester Faya amesema Watanzania wengi hasa wazee wanasumbuliwa na matatizo ya magoti na mifupa na hivyo kumuomba Dk Shah na uongozi wa hospitali yake uweze kushirikiana na hospitali za Tanzania na kubadilishana utaalam na teknolojia ili kuweza kuwasaidia kwa wingi wananchi wenye matatizo hayo, akisema taasisi iliyopo ya mifupa ya MOI pamoja na hospitali zingine binafsi zinazidiwa na wagonjwa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: