Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) anayemaliza muda wake, Jamal Malinzi ametoa kauli ya kukubali rasmi kuachia kiti hicho.

Hatua hiyo imekuja kutokana na kiongozi huyo kuwekwa rumande hadi Julai 3, mwaka huu mara baada ya kusomewa mashtaka yake mahakamani jana, jambo ambalo litamfanya akose nafasi ya kuhudhuria katika zoezi la usaili wa wagombea ambalo litafungwa kesho Julai Mosi.

Malinzi amezungumza kupitia wakili wake, Aloyce Komba kwamba anawashukuru watanzania kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote akiwa Rais, na kuwataka waelewe kuwa Soka la Tanzania bila Malinzi linawezakana.

Rais huyo anayekabiliwa na mashtaka takriban 28 yakiwemo ya utakatishaji fedha na kughushi nyaraka, amewataka wajumbe kuchagua mtu mwingine kwani anaamini kuwa kuna watanzania wengi wenye uwezo wa kuliongoza soka la Tanzania.

Kauli hiyo inaashiria kukubali kuachia nafasi hiyo, ikizingatiwa pia mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli alikwishaweka msimamo kuwa mchakato wa uchaguzi hautasimama, na kwamba yeyote ambaye hatatokea kwenye usaili atakuwa amejiengua mwenyewe.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: