1. Chukulia ni muda wa saa 1:25 jioni unarudi nyumbani peke yako, baada ya kazi ngumu zusizo za kawaida ofisini.

2. Umechoka sana, una hasira na umechanganikiwa.

3. Ghafla unajisikia maumivu makali kifuani yanaelekea mkononi na hata kwenye Taya. Upo umbali wa kama km5 tu kufika Hospitali iliyo karibu na kwako.

4. Bahati mbaya hujui kama utaweza kufika kwa unavyojisikia.

5. Ulishafundishwa kumfanyia mtu CPR, lakini aliyekufundisha hakuwaambia unaweza kujifanyia mwenyewe.

6. JINSI YA KIJISAIDIA UNAPOPATWA NA SHAMBULIO LA MOYO UKIWA PEKE YAKO.
Kwa kuwa watu wengi hupatwa na Shambulio la Moyo wakiwa peke yao bila msaada wowote, mtu ambaye mapigo yake ya Moyo hayako sawa na anaanza kuhisi kuzimia, au zimebaki sekunde 10 tu kabla hajapoteza fahamu.

7. Hata hivyo, waathirika hawa wanaweza kujisaidia kwa kujikoholesha mfululizo. Avute pumzi ndefu kila anapojikoholesha, na kikohozi lazima kiwe cha ndani mfululizo mpaka makohozi yatoke ndani ya kifua.

Kikohozi hicho kiendelee mpaka utakapopata msaada au mpaka mapigo ya Moyo yarudi kawaida tena.

8. Pumzi ndefu hupeleka Oksijeni mapafuni na kikohozi kuubana Moyo na kufanya mzunguko wa Damu uendelee. Nguvu ya kikohozi ya kuubana Moyo pia inasaidia kurudisha ktk mapigo ya kawaida. Kwa njia hii, waathirika wa shambulio la Moyo wanaweza kufika Hospitali.

Je tatizo hili husababishwa na nini?

Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).

Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?

Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na wale wenye umri mkubwa hususani kuanzia miaka 45 kwa wanaume na wanawake ni kuanzia miaka 55, wavutaji wa sigara, watu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zao.

Wengine walio katika hatari ni wale wenye kisukari, shinikizo la damu, walio na unene kupita kiasi (obesity), wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo zao (chronic renal failure), moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure).

Mbali na hao wengine ni wale wenye msongo wa mawazo, wanywaji wa pombe kupita kiasi, watumiaji wa madawa ya kulevya hasa ‘cocaine’ na ‘methamphetamine’ hali kadhalika na wale wenye upungufu wa vitamin B2, B6, B12 na folic acid.

Dalili za shambulizi la moyo
Dalili za tatizo hili ni maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto, kupumua kwa shida, kutoka jasho kwa wingi sana (diaphoresis), kuhisi mapigo ya moyo yanapiga haraka (palpitations), kichefuchefu na kutapika.

Sambamba na dalili hizo nyingine ni kupoteza fahamu na kuchoka haraka.

Kutoka kwa:-
Dr. FC Penal
(Cardiologist)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: