Mtafiti toka COSTECH, Bestina Daniel akitoa neno la shukrani.

Mwenyekiti wa CCM Igunga akitoa Maelekezo kwa maafisa Ugani wa Igunga

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Igunga akifunguzi mafunzo kwa Maafisa Ugani.

Maafisa Ugani wa wilaya Igunga wakiwa tayari kwa Mafunzo.

Na Hellen Isdory –Igunga Tabora.

Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Mkoani Tabora imewataka Maafisa Ugani katika Wilaya hiyo kufanya kazi zao kwa vitendo katika kuzalisha mazoa bora ya Biashara na chakula ili kutoa fursa ka wakulima katika kujipatia kipato kizuri na kuongeza pato la Taifa kupitia sekta hiyo ya Kilimo.

Kauli hiyo alitoa Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Peter Onesmo wakati akifungua mafunzo kwa maafisa ugani wa wilaya ya Igunga leo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya sayansi (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo (OFAB) ambayo yana lengo kuinua Zaidi uelewa wa matumizi bora ya kilimo cha kisasa.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa ipo haja kwa maafisa ugani hao kuchukulia mkazo mafunzo hayo hata kwa kushirikishana wenyewe kwa wenyewe katika kueleweshana na kutoa hari mpya ya kuweza kupata kilimo kilicho bora katika kata zao.

“Naanza kuweka Msukumo naomba mshirikishe mwenzio wa pembeni kwa kumuuliza pale ambapo haujaelewa katika masomo hayo ili uweze kutoka na ujuzi mzuri ambao utakusaidia kuwa na kilimo kilicho bora katika sehemu yako ya kazi” Alisema Onesmo.

“Baada ya Mafunzo haya tutaanza kufanya mashindano kwa kila kijiji na kata kwani tutakapotoka hapa kila mtu atarudi katika kata yake kwa hiyo nahitaji mashindano ili wakulima kunyonya utaalamu kutoka kwenu na kuanza kupata Mazao bora yenye Tija kwa Jamii”Aliongezea Onesmo

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilayani hapo Costa Ulomi alisema kuwa anafurahi kuona ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezwa na Jukwaa hilo kwa kuwa na Mafunzo ya kufikia kilimo cha Kisasa ambacho kitasababisha Tanzania kuwa nchi ya Viwanda.

“Nashukuru kuona Ilani ya CCM inatekelezwa kwa kupitia Mafunzo haya kwani hii ni sehemu ya utekelezeaji wa ilani ambapo ukienda katika mwelekeo wa 2010/2025 kwenye ilani haya mambo yameweka ya kukumbushana masuala mazima ya kilimo”

“Wilaya ya Igunga inalima kilimo ambapo isipo pata elimu ya kibaolojia ya kilimo tunaweza kukosa matokeo mazuri kama ilani ilivyoelekeza kwamba itaelekeza serikali yake itekeleze kutoa mafunzo ya kilimo ili kilimo kiwe cha kisasa na kiuchumi ili iwe malighafi ya viwanda kama mwelekeo wetu wa kuelekea 2025,” Aliongeza Ulomi.

Hata hivyo Mwenyekiti huyo alisema kuwa zao lililoko katika wilaya hiyo ni Pamba hivyo bado wanauhitaji Zaidi wa kuboresha zao hilo ili iwe tija kwa wilaya yao kutokana na ardhi yao.

“Kwa Igunga tunazao la pamba la kibiashara tunaomba sana wataalamu kupitia Wizara ya kilimo mtutazame sana kuendelea kuboresha mbegu ya pamba katika wilaya yetu ili zao hilo liwe malighafi ya viwanda kuelekea mwelekeo wetu wa nchi ya viwanda” Alisisitiza Ulomi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: