Familia ni Kanisa dogo la nyumbani, mahali pa sala na tafakari ya Neno la Mungu; mahali pa kuonjesha huruma, upendo na msamaha! Ni mahali ambapo wanafamilia wanakua na kukomaa, wanapokeana kusaidiana jinsi walivyo ili kuufikia utimilifu wa maisha. Lakini zaidi, familia ni kiini cha uinjilishaji unaofumbatwa katika ushuhuda makini wenye mvuto na mashiko! Changamoto kwa familia ya Mungu Barani Afrika ni kuhakikisha kwamba, inasimama kidete kulinda na kudumisha tunu msingi za maisha ya ndoa na familia kadiri ya mila na desturi njema za kiafrika. 

Kamwe nchi za Kiafrika zisikubali kuyumbishwa kwa kulazimishwa kukubali ndoa za watu wa jinsia moja, kwani huu si mpango wa Mungu katika maisha ya mwanadamu ni kinyume cha kanuni maadili na utu wema!

Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Dar es Salaam. Anasema, kuna mila na desturi za kiafrika ambazo zilikuwa na mafao ya kijamii kwa wakati fulani, lakini sasa zimepitwa na wakati. 

Kwa mfano ndoa za wake wengi, kwa sasa ni mila na desturi ambazo zimepitwa na wakati! Kumbe, kuna haja kwa watu wa Mungu Barani Afrika kujitamadunisha na hivyo kukubali kuipokea Injili ya Kristo ili iweze kusafisha mila na desturi zilizopitwa na wakati.

Kwa upande mwingine, Baba Mtakatifu Francisko katika Wosia wake wa kitume, “Amoris laetitia” yaani “Furaha ya upendo ndani ya familia” anasema kwamba, elimu na malezi kwa watoto ni wajibu msingi kwa wazazi, dhamana inayopaswa kutekelezwa kwa hekima, busara na uhuru. Wazazi na walezi wawe ni vyombo na mashuhuda wa katekesi makini wanayoishuhudia na kuwafundisha watoto wao kuipokea katika uhuru kamili.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: