Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour akijiandaa kuweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little Treasures leo Jumanne Julai 11,2017.
Jiwe la Msingi la Shule ya Msingi Little Treasures limewekwa na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa ndugu Amour Hamad Amour.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Kiondo akifungua mlango ili kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour (aliyevaa miwani) aingie ndani ya jengo hilo kuangalia vyumba vya madarasa.Wa pili kutoka kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Amour Hamad Amour (kushoto) akiwa katika moja ya madarasa ya jengo jipya la shule ya msingi Little Treasures.
Muonekano wa jengo hilo jipya la shule ya msingi Little Treasures lenye vyumba vinne vya madarasa.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour akizungumza katika shule ya msingi Little Treasures ambapo alisisitiza wazazi na walezi kusomesha watoto wao kwani elimu ndiyo msingi wa maisha yao.
Kulia ni Meneja wa shule ya Msingi Little Treasures Mwita Nchagwa na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures Paul Kiondo wakifuatilia hotuba ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017, Amour Hamad Amour.
Wanafunzi wakimsikiliza kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour.
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakiimba wimbo mbele ya kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka 2017,Amour Hamad Amour (kulia).
Wanafunzi wa shule ya msingi Little Treasures wakishika mwenge wa uhuru.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa mwaka 2017,Amour Hamad Amour ameweka jiwe la Msingi katika shule ya Msingi Little Treasures iliyopo katika kijiji cha Bugayambelele kata ya Kizumbi katika Manispaa ya Shinyanga.

Amour ameweka jiwe la msingi katika shule hiyo ya Binafsi inayotoa elimu ya awali na msingi leo Jumanne Julai 11,2017.

Akisoma taarifa fupi kwa ki ngozi huyo,Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Little Treasures, Paul Kiondo alisema mradi huo wa vyumba vine vya madarasa na matundu nane ya vyoo umegharimu shilingi 120,000,000/=.

“Jengo hili lenye kiwango na ubora wa hali ya juu ili kutoa mazingira bora ya ufundishaji na ujifunzaji, lina uwezo wa kubeba wanafunzi 180Madarasa haya manne ni kati ya 15 yaliyopo katika shule hii, ujenzi ulianza mwaka 2016 na umekamilika mwezi Juni 2017 ambapo shule imetumia rasilimali zake za ndani”,alieleza Kiondo.

“Hivi sasa tupo katika mchakato wa kujenga shule ya sekondari ili wahitimu wa shule hii watakaopenda waendelee na masomo ya sekondari hapa hapa,lengo letu ni kutoa elimu bora kwa wanafunzi wetu kwa mujibu wa matakwa na muongozo wa serikali yetu tukufu”,aliongeza Kiondo.

Naye Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa , Amour Hamad Amour alimpongeza mwekezaji aliyejenga shule hiyo kwa kuona umuhimu wa kuwekeza katika elimu na kuongeza kuwa serikali inatambua jitihada nzuri zinazofanywa na watu binafsi katika sekta ya elimu nchini.

"Serikali yetu inasisitiza viwanda,ili kufanikisha vizuri zaidi tunahitaji wataalamu wa kuendesha viwanda hivyo,hivyo tunapaswa kuwapa wanafunzi wetu elimu itakayowezesha kupata wasomi waliobobea katika viwanda",alisema Amour.

"Naomba uongozi wa shule ushirikiane na serikali kuhakikisha watoto wanapata elimu bora na elimu bora inategemea walimu bora,jukumu la uongozi wa shule kuhakikisha kuwa walimu wanaojituma ipasavyo katika ufundishaji",aliongeza Amour.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: