Tuesday, July 18, 2017

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU AKUTANA NA MTAFITI WA MAISHA YA SOKWE DKT. JANE GOODALL

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Mwanaharakati wa masuala ya mazingira na mtafiti wa maisha ya Sokwe katika Hifadhi ya Gombe mkoani Kigoma, Dkt. Jane Goodall. Dkt. Goodall pamoja na ujumbe wake walikutana na kuzungumza na Mhe. Makamu wa Rais Ikulu jijini Dar es Salaan. Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mhe. January Makamba pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Injinia Ngosi Mwihava.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu