Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimpa mkono wa pole Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe wakati wa ibada maalum ya kuaga mwili wa mke wake marehemu Linah George Mwakyembe kwenye kanisa la KKT Kunduchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa heshima za mwisho mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Linah George Mwakyembe mke Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe katika kanisa la KKT Kunduchi jijini Dar es salaam​.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Harisson Mwakyembe akilia juu ya jeneza la Mke wake Marehemu Linah Mwakyembe wakati wa kuaga mwili huo nyumbani kwake Kunduchi, Jijini Dar es Salaam mapema leo ambapo baadaye mwili huo ulisafirishwa kwenda Kyela, Mbeya kwa ajili ya mazishi.
Ibada ya kuombea mwili wa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe Harisson Mwakyembe, Marehemu Linah Mwakyembe ikiendelea katika kanisa la KKKT Kunduchi, Dar es Salaam kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda kyela, Mbeya kwa ajili ya mazishi.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe akitoa heshima yake ya pekee kwa kifo cha mkewe Linah Mwakyembe. (Picha kwa Hisani ya Times)
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: