Mkuu wa Wilaya ya Sikonge, Peres Magiri, akizungumza na maofisa ugani wa wilaya hiyo wakati akifungua mafunzo ya siku moja kwa maofisa hayo yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB), wilayani humo mkoani Tabora leo. Kutoka kushoto ni Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTECH, Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Hashim Kazoka na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pascal Ngunda.
Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Pascal Ngunda, akizungumza kwenye mafunzo hayo.
Mtafiti Bestina Daniel kutoka COSTECH, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Costech.
Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Renatus Mahimbali akizungumza.
Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia, Dk.Nicholaus Nyange akitoa mada kwa maofisa ugani hao.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Hashim Kazoka, akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu akizungumza.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), akizungumza. Kushoto ni Katibu wa CCM wa Wilaya, Emanuel Alex.
Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia, Dk.Nicholaus Nyange (kulia), akimkaribisha mgeni rasmi katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa wilaya hiyo, Peres Magiri wa tatu kulia.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Maofisa ugani.
Mafunzo yakiendelea.
Watoa mada wakisubiri kuwajibika. Kutoka kushoto ni Mshauri wa Jukwaa la Matumizi ya Bioteknolojia, Dk.Nicholaus Nyange, Mtafiti wa Mazao ya Kilimo kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ukiriguru mkoani Mwanza, Bakar Japhet, Mtafiti wa zao la pamba kutoka Ukiriguru Stellah Chilimi na Ofisa Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Said Babu.
Maofisa ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Dotto Mwaibale, Sikonge-Tabora

VIONGOZI wa Halmashauri wametakiwa kuacha kuwapa kazi za kiutendaji maofisa ugani badala yake wametakiwa kuachwa waendelee na shughuli zao za ugani ili kuinua kilimo.

Mwito huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Sikonge, Peter Nzalalila wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja kwa maofisa ugani wa wilaya hiyo mkoani Tabora leo asubuhi.

"Napenda kuwaeleza viongozi wa halmshauri wawaache maofisa ugani wafanye shughuli zao za ugani badala ya kuwapa kazi za utendaji ambazo zinapaswa kufanya na maofisa watendaji wa kata na vijiji" alisema Nzalalila.

Alisema ili kilimo kiweze kusonga mbele ni lazima wataalamu wa kilimo wakabaki katika kazi yao na si kufanya kazi za watendaji.

Nzalalila aliwataka maofisa ugani hao kila mmmoja kuwa na mpango wa kujua idadi ya wakulima katika eneo lake la kazi pamoja na mahitaji yao kama pembejeo ikiwemo mbolea ili iwe rahisi kujua mahitaji ya wakulima.

Alisema Mkoa wao umepata bahati ya pekee kwa wataalamu wake kupata mafunzo hayo ambayo yanalenga kuwaongezea ujuzi na kuwakumbusha majukumu yao.

Alisema wilaya inaamini mafunzo hayo yatasaidia kuinua kilimo cha kisasa katika wilaya hiyo na kuongeza uzalishaji wa mazo ya chakula kama mahindi, mihogo na mpunga.

Alisema mazao yote matatu ya chakula ya Mahindi,Mihogo na mpunga ni mazao muhimu kwa chakula kwa wakazi wa wilaya hiyo hivyo mafunzo hayo yawe chachu mpya katika kufanya mapinduzi kwenye kilimo na kuwataka kutumia mbinu hizo kuzalisha zao la biashara la Tumbaku kitaalmu kuwaandaa wakulima na mpango wa serikali ya viwada.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya hiyo Peres Magiri aliagiza pembejeo za Kilimo zikifikishwe kwa wakati kwa wakulima kabla ya kuanza mimu wa kilimo ili wakulima waweze kupata muda wa kuandaa mashamba yao.

Alisema iwapo pembejeo za kilimo zikimfikia mkulima kwa wakati itamsaidia kujiandaa vizuri kuliko kumcheleweshea jambo ambalo linamrudisha nyuma katika kilimo.

Magiri aliwataka maofisa ugani hao kupokea mafunzo na kuyapeleka wa wakulima ili kuwasaidia kupata mbinu mpya za uzalishaji na zinazotumia teknolojia za kisasa katika kuongeza tija kwenye uzalishaji wa mazao mbalimbali yanayolimwa kwenye maeneo yao.

Mtafiti Bestina Daniel kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Costech alisema mafunzo hayo yameandaliwa na Costech kupitia Jukwaa la Bioteknolojia kwa maendeleo ya kilimo nchini (OFAB).

“Tumeona tuendeshe mafunzo haya kwenu ili kuwakumbusha majukumu yenu na kuwapatia mbinu mbalimbali ili muweze kutekeleza majukumu yenu vizuri maana wakulima wanawategemea nyinyi kuwasaidia kupitia taaluma yenu hiyo” alisema Daniel Daniel.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: