Na MARIA SARUNGI.

Wakati wazee wetu walitumia kila walichoweza kuwakomboa watanzania waliokuwa wanakandamizwa na wakoloni, hawakujali kwamba wakoloni wana bunduki sisi tuna rungu hivyo tutakufa, hawakujali kwamba Maji hayazuii risasi, hawakujali Wao wanaongea Kiingereza sisi kiswahili, hawakujali wale wanavaa Nguo nzuri sisi tunavaa ngozi, hawakujali maslahi yao binafsi, waliweka mbele maslahi ya Taifa Kwa kizazi kijacho.

Leo tupo kwenye vita ya uchumi, vita ngumu. Tunaopigana nao ndio wanaotupa misaada, ndio waliotupa Elimu, ndio wanaoendesha teknolojia kote duniani, ndio wanaiamua nani aitwe dikteta na nani aitwe gaidi, ndio wenye mifumo yote ya Mahakama duniani, wenye uwezo mkubwa kivita.

Pamoja na hayo, licha ya kuwa tunahitaji mshikamano Wa kitaifa kuliko kipindi chochote kwenye historia ya nchi hii bado kuna watu wanaojiita watanzania wanakesha wakiomba Tanzania tushindwe na tulipishwe faini.

Kitendo cha Serikali kukubali mazungumzo na Barrick ambao ndio wanamiliki ACACIA Kwa asilimia kubwa, kimewafanya ACACIA kuonekana sio sehemu ya mazungumzo. ACACIA wameenda kufungua shauri katika Tume ya usuluhishi yaani arbitration (kulingana na press release yao) dhumuni kubwa ni Wao pia wawe sehemu ya mazungumzo. Kuna baadhi ya watanzania wameanza kushangilia eti tumeshitakiwa na tutalipishwa faini.

Ndugu zangu watanzania napenda kuwaambia hivi:

1. Kufungua kesi MTU yeyote anaruhusiwa, hata wewe unaweza kufungua kesi kupinga ujenzi Wa reli ya SGR.
Wapo walioenda kufungua kesi Mahakama za kimataifa kupinga uchaguzi Wa Tanzania.
Ninachomaanisha hapa unaweza kufungua kesi japo matokeo ya kesi ni probability.

2. Hata tukishitakiwa tuko tayari ilimradi tuvunje hii mikataba ambayo itaendelea kutunyonya miaka zaidi ya 80 inayokuja

3. Napenda kuwakumbusha, serikali ikipigwa faini yoyote hawatalipa Ccm, watalipa watanzania wote, sasa endeleeni kuleta ushabiki Wa kisiasa.

4. Tuwe na uzalendo ndugu zangu, tuache kutumia matatizo kama chanzo cha kujipatia umaharufu au Ku prove theory.

Wazee wetu wakitafuta Uhuru, wengi walikufa lakini lengo lilitimia na mpaka sasa tuna kula matunda yao.

Mhe. Rais Kanyaga twende, hata kama mkate tutanunua Kwa sh laki 3, mbona Zimbabwe walivuka Salama pamoja na vikwazo vyote walivyowekewa, Leo Zimbabwe bado IPO na inaheshimika duniani kote.

Viva Magufuli Viva
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

1 comments: