Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akionyesha baadhi ya picha za watuhumiwa wa uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri kwa waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao na viongozi wa ngazi za juu wa Jeshi la Polisi ambapo alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Kulia ni Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP),Simon Sirro.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini(IGP), Simon Sirro, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), baada ya kufanya kikao kuhusiana na uhalifu katika maeneo ya Kibiti,Mkuranga na Ikwiriri,mkoani Pwani, ambapo Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kushoto),alitangaza kutafutwa kwa watu 16 wanaotuhumiwa kuhusika na uhalifu huo.Mkutano huo umefanyika katika Ukumbi wa polisi makao makuu,jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.
---
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Yussuf Masauni ametangaza kuwa, Jeshi la Polisi linawaska watuhumiwa 16 wa mauaji ambayo yamekuwa yakiendelea kufanyika katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji Mkoani Pwani kwa muda mrefu sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Masauni amesema kuwa watuhumiwa hao wanafahamika na tayari jeshi la polisi lina picha za watuhumiwa wote ambao wanasakwa.

“Nchi yetu ipo katika changamoto ya matukio katika maeneo ya Kibiti na Rufiji, ambapo matukio haya wakati mwingine yanaripotiwa ndivyo sivyo na vyombo vya habari na kusababisha hofu kwa wananchi. Sisi kama serikali lazima tuwatoe hofu wananchi wetu. Tuwaombe wanahabari mfikishe ujumbe sahihi zaidi.

“Jana tulifanikiwa kuwadhibiti wahalifu wawili kabla hawajatekeleza uhalifu wao, kwa hiyo jeshi letu linafanya kazi vizuri sana. Suala la kumaliza uhalifu wa Kibiti ni la lazima wala sio la mjadala tena.

“Maandalizi ya mkoa Mpya wa Kipolisi wa Rufiji yamekamilika na Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo tayari ameshateuliwa,” alisema Masauni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: