Toyota VX lenye namba za usajili T329 DGK alilokuwa akisafiria Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Ruvuma, Sikudhani Chikambo iliyopata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja leo mchana eneo la Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro.
MBUNGE wa Viti Maalum mkoa wa Ruvuma CCM, Sikudhani Chikambo amenusurika kifo katika ajali ya barabarani hii leo Dumila, Wilaya ya Mvomero, mkoani Morogoro. Anaandika John Nditi-Morogoro.
Mbunge huyo pamoja na watu wengine watano walikuwa wakisafiri kutoka Dodomna kwenda jijini Dar es Salaam ndipo gari walilokuwa wakisafiria Toyota VX lenye namba
za usajili T329 DGK, kupasuka gurudumu na kuacha njia na kupinduka na kusababisha kifo cha ndugu wa Mbunge huyo.

Akizungumza akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alikolazwa kwa matibabu alisema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wake kuwepa shimo lakini kutokana na ukubwa wa shimo hilo gurudumu lilitumbukia na kupasuka kisha gari kupoteza muelekeo na kupinduka mara tano.

“Dereva alikuwa anakwepa shimo, lakini kutokana na ukubwa wa shimo tairi lika tumbukia na kupasuka gari iliyumba na kupoteza mwelekeo na kupinduka mara tano kabla ya kusimama,”alisema Sikudhani.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: