Mbunge wa Kawe jioni la leo amekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni kufuatia agizo la Mkuu wa Wilaya la kutaka akamatwe kufuatia matamko ya kumkashfu Rais Dkt. John Pombe Magufuli aliyoyatoa jana wakati alipofanya mkutano na waandishi wa habari.

Katibu wa CHADEMA jijini Dar es Salaam, Henry Kilewo amesema Mbunge huyo wa Kawe na Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la CHADEMA (BAWACHA), ni kweli amekamatwa na Polisi na kupelekwa kituoni Oysterbay.

Kamanda wa Polisi, mkoa wa Kinondoni, Suzan Kaganda amesema amefanya hivyo kwa amri ya mkuu huyo wa wilaya.

“Wapi kakamatwa? Sisi tunachojua ni kuwa tunatekeleza agizo la Mkuu wa wilaya mengine muulize kamishna wa kanda maalum, nimetimiza wajibu wangu,” amesema.

Hii ni MESEJI yake mara baada ya kukamatwa!

"Wamekuja polisi kunichukua home! As we speak naelekea kituo cha polisi, probably Oysterbay Au Central. Wasaidizi wangu watakuwa na taarifa zaidi za ninakoelekea!

Mapema leo, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Ally Hapi alitoa agizo la kukamatwa kwa Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima James Mdee mara moja kwa kosa la kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

DC HAPI AIAGIZA POLISI KUMTIA MBARONI MBUNGE HALIMA MDEE
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi ameliagiza jeshi la Polisi Kinondoni kumkamata Mbunge wa Kawe Halima Mdee kwa kosa la kutoa kauli za matusi, dhihaka na uchochezi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi kwa ujumla.

Hapi ameagiza mbunge huyo kukamatwa, kukaa korokoroni kwa saa 48, kuhojiwa na kuchukuliwa hatua nyingine za kisheria kwa maneno aliyoyatoa jana akiongea na waandishi wa habari makao makuu ya Chadema mtaa wa Ufipa.

Hapi amesema kuwa maneno aliyoyatoa Mdee ni matusi yenye lengo la kuleta uchochezi unaoweza kuhatarisha amani na utulivu.

"Sitamvumilia mwanasiasa yeyote atakayethubutu kutoa kauli za matusi dhidi ya Mhe. Rais, au zenye kutaka kuleta uchochezi katika wilaya yangu."

Alisema DC Hapi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: