….wakionesha vyeti vya ndoa yao mara baada ya kuvisaini na kukabidhiwa.
Profesa Jay akiwa na mkewe kipenzi, Grace Mgonjo, mara baada ya kufunga ndoa katika kanisa la St. Peters, Mbuyuni jijini Dar es Salaam. Picha zote kwa hisani ya Global Publishers.

Profesa Jay amefunga ndoa katika Kanisa la Mtakatifu St. Peters Oysterbay jijini Dar es salaam leo Jumamosi Julai 08, 2017 na mpenzi wake wa siku nyingi Grace Mgonjo.

Cherekochereko za tukio kubwa la Mbunge wa Jimbo la Mikumi kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule almaarufu Profesa Jay limetikisa Jiji La Dar baada ya kufuatiliwa na watu wengi. Ndoa ya Profesa Jay na mpenzi wake wa muda mrefu. Kabla ya ndoa hiyo iliyoibua shangwe kwa ndugu, jamaa na marafiki waliofurika kanisani hapo, msafara wa kuelekea kanisani ulianzia nyumbani kwa Profesa Jay, Kimara-Temboni jijini Dar.

“Namshukuru Mungu nimetimiza ahadi ya ndoa kwa mchumba wangu ambaye tumepitia mabonde na milima,” alisema Profesa Jay baada ya kutoka kanisani hapo.

Ndoa hiyo ilifuatiwa na sherehe iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
…Grace akiingia kanisani kwa ajili ya kufunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Profesa Jay.
…Profesa Jay akiwa ameketi na mkewe muda mfupi baada ya kuingia kanisani tayari kwa tukio takatifu.
…wakipewa mkono wa dua mara wakati wakikamilisha tendo la Ibada ya Ndoa.
…Grace akipewa mkono wa pongezi na baraka mara baada ya kufunga ndoa.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: