Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry (wa tatu kutoka kushoto) akimpokea mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack (wa pili kushoto) kwa ajili ya kushiriki mkutano mkuu waJumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kanda ya ziwa mwaka 2017 uliofanyika katika Kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry akimkaribisha mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack na wageni mbalimbali waliohudhuria mkutano huo.
Waumini wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya na wananchi wenye mapenzi mema wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea katika mkutano huo.
Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya nchini Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame akitafsiri kwa lugha ya Kiswahili hotuba ya Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry aliyokuwa anaitoa kwa lugha ya Kiingereza wakati wa mkutano huo katika kijiji cha Sungamile.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack akitoa hotuba yake wakati wa kutano mkuu waJumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kanda ya ziwa mwaka 2017.
Viongozi mbalimbali wa serikali wakiwa eneo la tukio.Kulia ni Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Muliro Jumanne Muliro akifuatiwa na Afisa Uhamiaji mkoa wa Shinyanga Anna Maria Yondani.
Akina mama wakiwa eneo la mkutano.
Viongozi mbalimbali wa serikali ya mkoa wa Shinyanga na viongozi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea wakati wa mkutano huo.
Mkutano unaendelea.
Muonekano wa Msikiti wa Ahmadiyya Muslim Jamaat Tz Masjid Fath uliopo katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
---
Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Kanda ya Ziwa (Ahmadiyya Muslim Jamaat Kanda ya ziwa) leo Jumapili Julai 9,2017 imefanya mkutano wa mwaka wa Jumuiya hiyo kwa mwaka 2017.

Mkutano huo umefanyika katika Msikiti wa Ahmadiyya Muslim Jamaat Tz Masjid Fath uliopo katika kijiji cha Sungamile kata ya Mwalugulu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack aliyekuwa ameambatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa huo.

Akizungumza wakati wa mkutano huo,Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Maulana Sheikh Tahir Mahmood Chaudhry alisema uislamu ni amani hivyo lengo la mkutano huo ni kuhamasisha amani katika jamii kwa kuwakumbusha waumini kumjua mwenyezi mungu.

Alisema endapo jamii itakuwa na hofu ya mungu itasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza hata kumaliza kabisa vitendo viovu katika jamii ikwemo mauaji ya watu wasio na hatia kama vile vikongwe na watu wenye ualbino.

Katika hatua nyingine Sheikh Chaudhry alisema Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya ipo katika nchi 209 duniani ikiwemo Tanzania na mpaka sasa wamejenga misikiti 25 katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu.

“Jumuiya hii imeingia Tanzania takribani miaka minne iliyopita,kupitia mikutano yetu huwa tunaihamasisha jamii kuishi kwa amani,kufundisha watu watende mambo mema lakini pia tunaweka umeme wa jua na kuchimba visima katika vijiji ambavyo tumejenga misikiti yetu”,aliongeza.

Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya Tanzania Abdulrahman Mohammed Ame alisema sifa kuu ya uislam ni kuishi kwa amani na binadamu wengine na wala siyo kutisha watu wengine.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuendelea kuhamasisha amani katika jamii na kutoa mafunzo kwa waumini wao kama wanavyotamka na si vinginevyo.

“Viongozi wa dini mna jukumu la kuihamasisha jamii kuzuia makundi yasiyofaa katika jamii,toeni mafunzo yenye kujenga jamii na watanzania muwe tayari kutoa ushirikiano pale mnapoona kundi la watu flani wanataka kuleta uvunjifu wa amani”,alieleza Telack.

Aidha mkuu huyo wa mkoa aliipongeza Jumuiya ya Waislam wa Ahmadiyya kwa jitihada inazofanya katika kuhubiri amani katika jamii na kukemea vitendo viovu ikiwemo kuua watu wasio wakiwemo wazee na watu wenye ualbino pia kunyanyasa wanawake na watoto katika jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: