Monday, July 10, 2017

MTANGAZAJI WA EFM, SETH KATENDE AFARIKI DUNIA KATIKA HOSPITALI YA TAFA YA MUHIMBILI - DAR

Mtangazaji wa kituo cha radio EFM cha Jijini Dar es salaam ambaye alikuwa anatangaza kipindi cha Ubaoni Seth Kitende maarufu kwa jina ‘Bikira wa Kisukuma’ amefariki dunia leo jioni Jumapili Julai 9, 2017.

Taarifa za awali zinasema Seth amefariki akiwa kwenye Hospitali ya taifa Muhimbili baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Seth Katende alijipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii Tanzania akifahamika kwa jina la ‘Bikira wa Kisukuma’ ambapo baadae alianza kufanya kazi ya Radio kwenye kituo cha EFM.

Msiba upo nyumbani kwa baba yake Changanyikeni Dar es salaam.

Uongozi mzima wa Kajunason Blog unapenda kuwapa pole ndugu, jamaa na marafiki kwa msiba huu. Bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake libarikiwe. 

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu