Meneja Mkuu wa Efm Tanzania na TVE Tanzania, Dennis Ssebo ametoa ratiba kamili ya mazishi ya mtangazaji wa EFM, Seth Katende 'Bikira wa Kisukuma' kwenye makazi ya milele.

Kwa mujibu wa Sebbo, mazishi ya Sethi yatafanyika Jumatano ya Julai 12, 2017 saa nne asubuhi kwenye Viwanja vya Leaders ambapo misa ya kumuombea itafanyika kisha shughuli ya kuuaga mwili itafuatia kabla ya baadaye kwenda kwenye Makaburi ya Kinondoni, atakapoenda kuzikwa.
Mtangazaji wa EFM, Seth Katende almaarufu Bikira wa Kisukuma enzi ya uhai wake.

Bikira wa Kisukuma, alifariki juzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kwa mujibu wa baadhi ya wafanyakazi wenzake ambao hawakutaka kutajwa majina yao kwa vile siyo wasemaji, walisema marehemu alianza kuugua kiasi cha mwezi mmoja uliopita na msiba uko nyumbani kwa baba yake mzazi huko Changanyikeni.

Marehemu ambaye alikuwa akitangaza kipindi cha Ubaoni, kinachorushwa na redio hiyo kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa, saa kumi jioni.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: