Monday, July 17, 2017

NGOMA AFRICA BAND A.K.A FFU - UGHAIBUNI KULIAMSHA DUDE BONN, UJERUMANI

 Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band aka FFU-Ughaibuni au Viumbe wa ajabu "Anunnaki Aliens" yenye makao yake nchini Ujerumani inatarajiwa kutumbuiza katika onyesho la wazi la Orient-Afrika litakalo fanyika mjini Bonn,Ujerumani siku ya Ijumaa 28. Julai 2017 saa 2.00 Usiku(20.00 hrs), bendi hiyo inayoongozwa na Kamanda Ras Makunja inadumu katika medani ya muziki kwa miaka 24 na kufanikiwa kuteka washabiki wa kimataifa,pamoja na kuachia nyimbo na CD kadha bendi hiyo imejizolea umaarufu katika majukwaa ya kimataifa wa mdundo wa Extraordinary "Bongo Dansi" unaowatia kiwewe washabiki barani ulaya. Usikose kujumuika nao at www.ngoma-africa.com au www.instagram.com/ngomaafricaband 

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu