Wamiliki wa bendi ya FM Academia “Wazee wa Ngwasuma” wametoa ufafanuzi juu ya kile kilichopekea Nyoshi el Saadat kuvuliwa cheo cha urais wa bendi.

Wiki mbili zilizopita Nyoshi alivuliwa cheo hicho alichokitumikia kwa takriban miaka 20 na nafasi yeke kuchukuliwa na Patcho Mwamba, hatua ambayo imezua fikra tofauti miongoni mwa mashabiki wa muziki wa dansi – wengine wakiona Nyoshi kaonewa na wengine wakiunga mkono mabadiliko.

Blake Mwambona ambaye amejitambulisha kama mdogo wa aliyekuwa mmiliki wa FM Academia (Marehemu Martin Kasyanju), amesema kwamba kwa zaidi miezi sita iliyopita, maendeleo ya bendi yamekuwa yakididimia kwa kasi kuwa, ikiwa ni pamoja kukosekana ari kwa wanamuziki wengi.

Mwambona amesema wanaamini mfumo wa kubadilishana uongozi, ndio bora zaidi badala kumsimika mtu uongozi kwa miaka mingi na mwisho wa siku anageuka kuwa mtawala.

Naye Nsajigwa Martin Kasyanju ambaye ni mtoto wa marehemu Martin Kasyanju, amesema kuwa wao hawajamfukuza Nyoshi, ila akiamua kuondoka hawana kizuizi.

Tayari imedaiwa kuwa Nyoshi yuko chimbo akisuka bendi yake mpya na hajakanyaga show za FM tangu avuliwe urais wa bendi.

Katika mahojiano yake na Jembe FM ya Mwanza wiki mbili ziliyopita, Nyoshi alifunguka kuwa ameachana na FM Academia na ataibuka na bendi mpya.

“Hatujamfukuza, tumebadili uongozi wa bendi kwa manufaa ya biashara yetu, kama yeye hawezi kuishi FM bila cheo cha urais, hatutakuwa na namna ya kumsaidia. Kwetu sisi biashara kwanza halafu mambo mengine baadae", Japo yanasemwa mengi, hata hivyo sisi tunatambua Nyoshi bado ni muajiriwa wa FM Academia kama mikataba inavyojieleza na taratibu za kazi zilivyo, anaeleza Nsajigwa.

“Tunathamini sana mchango wa Nyoshi, lakini ni lazima ifahamike kuwa FM Academia inafanya biashara, kuna wakati maamuzi magumu lazima yachukuliwe kwaajili kulinda biashara” aliongeza Nsajigwa na kufichua kuwa mabadiliko hayo yameongeza furaha, amani na ari kwa wanamuziki wa FM Academia.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: