Kristo Yesu katika maisha na utume aliwahubiria watu kwa kutumia lugha na mifano ya kawaida iliyozoeleka na watu ili kuweza kufikisha ujumbe wa Neno la Mungu kwa watu wengi zaidi. Alitamani kuona kwamba, Neno la Mungu linagusa nyoyo za watu ikilinganishwa na lugha iliyokuwa inatumiwa na viongozi wa wakati ule, iliyokuwa ngumu na kuwafanya watu kuwakimbia.

Baba Mtakatifu anaendelea kusema kwamba, Neno la Mungu, linawaalika waamini kujichunguza kutoka katika undani wao; ili kuwa na ujasiri wa kumshukuru Mungu kwa udongo mzuri ambao bado uko ndani mwao unaoweza kuzaa matunda mema na kuendelea kujibidisha kuboresha nyoyo ambazo zinaelemewa na malimwengu. 

Wajitahidi kuangalia ikiwa kama nyoyo zao ziko wazi kupokea kwa imani na matumaini mbegu ya Neno la Mungu. Wawe na ujasiri wa kuondoa vilema vya maisha ya kiroho kwa njia ya: toba na wongofu wa ndani; kwa kukimbilia huruma na upendo wa Mungu katika Sakramenti ya Upatanisho; kwa sala na matendo ya huruma: kiroho na kimwili.

Hapa, Baba Mtakatifu Francisko anawaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kuangalia mioyo yao, ili hatimaye, waweze kutambua ni mambo yepi yanayokwamisha mbegu ya Neno la Mungu kutozaa matunda kwa wakati wake? Mwishoni, Baba Mtakatifu Francisko amewaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kumkimbilia Bikira Maria wa Mlima Karmeli, aliyeonesha mfano bora na wakuigwa kwa kulipokea Neno la Mungu na kumwilisha katika uhalisia wa maisha yake, awasaidie kutakasa nyoyo zao, tayari kutoa nafasi ya kuhifadhi uwepo wa Mungu katika maisha yao.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: