Monday, July 3, 2017

PPF WAJIZOLEA SIFA YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANACHAMA NA WANANCHI WANAOTEMBELEA KATIKA MAONESHO YA SABASABA 2017

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. William Erio, (mwenye suti), akiungana na wafanyakazi wenzake kuhudumia wananchi wakati wa maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam Julai 2, 2017. Wananchi wengi waliotembelea banda hilo wamefurahishwa na huduma zitolewazo na wafanyakazi wake kwa kwa jinsi wanavyosikiliza na kutoa huduma kwa wanachama na wananchi wengine. miongoni mwa maswali mengi yaliyoulizwa mara kwa mara ni kuhusu mpango wa uchangiaji wa hiari ujulikanao kama "Wote Scheme), unaotoa fursa kwa wajasiriamali wadogo kama mama lishe madereva wa bodaboda, wamachinga na mtu yeyote anayefanya kazi halali ya kumuingizia kipato anavyoweza kujiunga na mpango huo na hatimaye kupata faida mbalimbali ikiwemo bima ya afya na mikopo kwa wajasiriamali wadogo,
Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
Meneja wa elimu kwa wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw. Kwame Temu, (kushoto), akitoa maelezo kwa mwananchi huyu aliyetembelea banda la Mfuko huo lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere kuinakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam leo Julai 2, 2017
Wananchi wakipatiwa maelezo kuhusu shughuli na huduma zitolewazo na PPF.
Wafanyakazi wa PPF, wakiwa makini katika kuwahudumia wananchi waliofika banda la Mfuko huo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu