Bw. Johanes Bukwali, Katibu Tawala Msaidizi Uchumi na uzalisha Sekretarieti ya mkoa wa Mwanza, akisoma Hotuba ya Katibu Tawala wa Mkoa huu wakati wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Siku nane kuhusiana na PlanRep kwa watendaji wa a Mikoa ya Kanda ziwa
Baadhi ya Watengenezaji wa Mfumo Mpya wa PlanRep, ambao wataufundhisha kwa muda wa siku nane Mkoani Mwanza, hapa wakijitambulisha mbele ya Watendaji walifika kwaajili yakufundishwa.
Watendaji wa PS3 wakifatilia kwa Makini Hotuba wakati wa ufunguzi wa Semina ya PlanRep
Bw. Desderi Wengaa,Mkuu wa Masuala ya Mifumo kutoka PS. akitoa maelezo ya Utangulizi kabla ya kufunguliwa kwa Semina hiyo inayofanyiaka Mkoani Mwanza.
Bw. Elias Rwamiago, Kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI akizunguza kabla yakumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua Senina hiyo ya Siku nane.

Na Atley Kuni- Mwanza.

Serikali mkoani hapa imesema, Mfumo mpya wa kuandaa Mipango na Bajeti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa, ulioboreshwa utakuwa msaada kwa Mwananchi kwani utaweza kumshirikisha moja kwa moja wakati wakuibua vipaumbele vya maendeleo katika maeneo yao.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, C P. Clodwig Mtweve, wakati akifungua mafunzo ya siku nane yaliyo andaliwa na TAMISEMI kupitia mradi wa Wamarekani wa kuimarisha mifumo yaani PS3 kwa watendaji wa Serikali kutoka katika mikoa ya kanda ya ziwa.

Katika hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala msaidizi upande wa uchumi na uzalishaji, Johanes Bukwali, amesema mfumo mpya wa PlanRep uliboreshwa unaenda kutumika kuanzia ngazi ya msingi yaani vituo vyetu vya kutolea huduma ambapo utawezesha kuandaa mipango na bajeti kutokana na vipaumbele na mahitaji ya wananchi.

Ameongeza kuwa,” kwa kutumia mfumo wa zamani wa PlanRep, ulikuwa huwezi kuainisha mipango na bajeti za kituo kimoja kimoja kwa kuwa mipango yote ilikua ikiishia kwenye ngazi ya Halmashauri, hali ambayo ni tofauti na sasa katika mfumo hu mpya wa PalnRep”.

Bukwali amesema kwamba, PlanRep iliyoboreshwa imefanyia kazi changamoto zilizokuwepo kwa kuhakikisha kwamba mpango na bajeti unaingizwa kwa kila mtoa huduma, na unaingiza namba za utambulisho kwa kila mtoa huduma mmoja mmoja kwa kila sekta. Vile vile, mfumo huu umeweka nafasi ya kila mtoa huduma kuainisha matokeo yaliyotarajiwa (Service Outputs), amesisitiza Bukwali.

Bukwali amemalizia kwakuwashukuru sana PS3 kwa mafunzo hayo, maana kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) ambao tayari wamekuwa wanafanya kazi kwa karibu sana na Serikali ya Tanzania.

Kwa upande wake mwakilishi wa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa, Elisa Rwamiago, amewataka washiriki hao kujifunza kwa umakini na kuulewa mpango huo ili katika mwaka ujao wa fedha wa 2017/2018 waweze kuutumia katika kuandaa Bajeti zao.

Awali akizungumza Mwakilishi kutoka PS3 Desderi Wengaa, amesema wao kama PS3, ambao wanafanya kazi katika Mikoa 13 na Halmashauri 93 nchini, wanachotaka kuona ni matokeo chanya kwa kile wanacho kifanya.

“Mfumo mpya wa PlanRep ni wa kitaifa na uko kwenye toleo la mfumo wa kielektroniki ambao unatambulisha teknolojia ya mawasiliano na kufanya upatikanaji wake kuwa rahisi mahali kokote na muda wowote” alisema Desderi.

Ameongeza kuwa, Mipango na bajeti za vituo vya kutolea huduma kwa wananchi itaonekana kupitia mfumo wa PlanRep kwa kuongeza ufanisi, uwazi na uwajibikaji kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma kwa wananchi wa Tanzania.

Aidha amefafanua kuwa PlanRep itatumika katika sekta zote za umma na imehuishwa na mifumo mingine ya Serikali ili kuboresha usimamizi na kuwezesha Serikali katika ngazi zote kuweza kufanya kazi vizuri ili kutoa huduma bora kwa jamii.

Mafunzo hayo kwa awamu ya kwanza yanafanyika katika kanda mbili, za Mwanza pamoja na Mtwara, na kwamba yanajumuisha watumiaji wa mifumo hiyo ambao ni Waganga Wakuu, Makatibu wa Afya, Maafisa TEHAMA na Wachumi kutoka ngazi ya Mkoa kwa upande mmoja, pamoja na Waganga Wakuu, Maafisa Mipango, Wahasibu, Wachumi, na Maafisa TEHAMA wa Halmashauri kwa upange mwingine, ambao wahusika katika kuandaa mipango na bajeti za Halmashauri kutokana na taarifa zilizokusanywa kutoka vitengo mbalimbali ndani ya Halmashauri zao.

Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: