Kwa mara nyingine tena shirika la UZIKWASA lililopo wilayani Pangani limekuja na mambo mapya. Safari hii ni tamthilia ya mchezo wa redio unaofahamika kama Tamapendo. Lengo la tamthilia hii ni kuonesha changamoto za vijana wawili kujiendeleza katika maisha yao katika jamii ambapo kanuni za unyanyasaji wa kijinsia za kijamii bado zinashinda.

Tamapendo inakuwa tamthilia ya pili ya redio kutengenezwa na shirika la UZIKWASA baada ya mchezo wa redio wa Penye Nia…..uliopatwa kusikilizwa na jamii nzima ya Pangani kupitia kituo cha redio cha Pangani FM, ambacho pia kinamilikiwa na shirika la UZIKWASA wilayani Pangani.

Shirika hili pia limekuwa na utaratibu kutengeneza filamu mbali mbali hasa kuhusu maswala ya haki na ukatili wa kijinsia. Kutokana na utafiti wa ndani kabisa filamu za UZIKWASA zinasimulia story halisi za jamii ya Pangani na zilifanikiwa kugusa watamazaji kwa sababu filamu hizi ni kama kioo cha changamoto zao.

Filamu hizo ni Fimbo ya Baba ambayo ilitengenezwa mwaka 2006, Chukua Pipi iliyotoka 2012 na filamu maarufu ya AISHA ya mwaka 2015. AISHA ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa, siyo Pangani tu, lakini Tanzania nzima na nchi nyingi za kimataifa. Imepata tuzo mbalimbali kimataifa kutoka tamasha za filamu maarufu USA na Africa.

Pamoja na hayo yote, sasa shirika la UZIKWASA limekuja tena na tamthilia la redio inayoitwa Tamapendo. Kama kawaidi ya filamu na tamthilia ya redio za UZIKWASA karibu waigizaji wote hutokea Pangani. Na ndivyo ilivyotokea kwa Tamapendo ambayo imeongozwa kwa ushirikiano na wagurugenzi wa mchezo Chande Omar na Irene Sanga. Story ya tamthilia hii inatokana na tafiti iliofanika na UZIKWASA pamoja na mchango wa wanajamii wa Pangani.

Tamthilia imetengenezwa na kuhaririwa kwenye studio ya redio Pangani FM –Sauti ya Jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: