Treni aina ya Rovos Rail ambayo inashikilia nafasi ya pili kwa ufahari duniani ikiwa imewasili kutokea Cape Town nchini Afrika Kusini na watalii wapatao 65 mpaka TAZARA jijini Dar es Salaam.
Wageni wakishuka.
Na Kajunason Blog/Cathbert Kajuna.

Kuwasili kwa watalii 65 kwa treni inayoshikilia nafasi ya pili kwa ufahari duniani 'Rovos Rail' kumeendelea kuiweka Tanzania katika nafasi nzuri ya kutangaza sekta ya utalii kwa njia ya reli.

Akizungumza katika mapokezi yaliyofanyika TAZARA jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania, Devitha Mdachi amesema fursa kama hizo zinapojitokeza ni vyema kuzitendea haki na kuwakarimu wageni.

Bi. Mdachi amesema kuwa TTB imeona kuwa utalii wa njia ya reli ni moja ya Utalii ambao unaweza kuhamasisha utalii wa ndani na ndiyo maana wameanza ushirikiano na reli ya TAZARA katika kuanzisha safari maalumu kwa ajili ya wataalii wa ndani kutembelea vivutio vya nchi hasa vilivyoko kusini mwa Tanzania.

Watalii hao waliofika nchini Tanzania wanatarajia kuelekea Zanzibar na maeneo mengine ya vivutio vya nchi kabla ya kurudi makwao.

Kwa Habazi zaidi Tembelea TRAIN SAFARIS
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: