Monday, July 31, 2017

VIGOGO TFF, SIMBA WARUDISHWA RUMANDE

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imehairisha kesi inayomkabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamali Malinzi na wenzake hadi August 11,2017 kwa sababu upelelezi haujakamilika.

Wakili wa serikali, Nassoro Katuga ameieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi haujakamilika, hivyo anaomba kesi ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Malinzi na wenzake wanakabiliwa na makosa ya utakatishaji fedha kwahiyo kesi yao kukosa dhamana na Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri ameahirisha kesi hiyo hadi August 11, 2017.

Wakati huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kesi inayowakabili viongozi wa Klabu ya Simba Rais Evanve Aveva na Makamu wake Nyange Geofrey Kaburu hadi  August 7, 2017 kutokana na upelelezi wa kesi kutokamilika.

Hata hivyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa ameutaka upande wa mashtaka uliowakilishwa na wakili Leornad Swai kuharakisha upelelezi.

Watuhumiwa wote wamerudishwa rumande mpaka August 7 kesi yao itakaposikilizwa

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu