Muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk.Nicku Kyungu akihubiri katika kongamano la kitaifa la viongozi wa dini lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi Ubungo jijini Dar es Salaam leo.
Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dodoma, akifundisha katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maombi hayo, Askofu Mkuu wa Naoith Pentekoste Church, Dk.David Mwasota akizungumza katika kongamano hilo.
Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria alifundisha somo la watu kuwa waaminifu katika kila jambo.
Usikivu katika kongamano hilo
Maombi yakifanyika.
Maombi yakiendelea.
Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria akitoa zawadi ya vitabu kwa maaskofu.

Na Dotto Mwaibale

VIONGOZI wa dini wametakiwa kutumia taaluma waliyonayo kumsaidia Rais Dk. John Magufuli kuliletea taifa maendeleo na kuondokana na umaskini nchini.

Mwito huo umetolewa na muhubiri wa kimataifa 'Mama Afrika' Dk.Nicku Kyungu wakati akihubiri katika kongamano la kimataifa la viongozi wa dini lililofanyika Kanisa la Naoith Pentekoste Church Makuburi jijini Dar es Salaam leo.

Alisema viongozi wa dini waliopo katika makanisa wanataaluma mbalimbali hivyo mbali ya kuhubiri neno la mungu wanapaswa kutumia taaluma walizonazo kumsaidia Rais katika maendeleo ya nchi jambo litakalosaidia nchi kuondokana na umaskini na adui ujinga.

Dk. Kyungu alisema katika imani Tanzania sasa imetoka katika uchanga na sasa inakwenda mbele na hilo ni jambo la kujivunia.

Alisema nchi ya Tanzania imebarikiwa tangu uongozi wa baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Ali Hassan Mwinyi, Benjamini Mkapa, Jakaya Kikwete na sasa Dk. John Magufuli.

"Ili ni jambo la kujivunia kwa nchi kuwa na amani tangu wakati huo hadi leo hii na ndio maana tumeona ni vizuri tukafanya maombi ya shukrani ya kuliombea taifa na Rais wetu yatakayofanyika Jumamosi Uwanja wa Uhurua jijini Dar es Salaam kuanzia asubuhi" alisema Dk. Kyungu.

Dk. Kyungu alisema kauli alioianzisha Rais Magufuli ya Hapa Kazi Tu ipo katika biblia hivyo ni wajibu wa kila mtu kufanya kazi kama mungu alivyomuagiza adamu pale bustani ya hedeni.

Katika kongamano hilo ambalo litakwisha kesho viongozi mbalimbali wa dini na maaskofu kutoka ndani na nje ya nchi walipata fursa ya kuhubiri ambapo Mchungaji Timoth Joseph kutoka Nigeria alifundisha somo la watu kuwa waaminifu katika kila jambo.

Mchungaji Dk. William Kopwe wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania kutoka mkoani Dodoma alisema kanisa hivi sasa limeingiliwa na magonjwa likiwemo la waumini kuwanenea mabaya viongozi wao.

Maombi hayo ya shukrani kitaifa yatakayofanyika Jumamosi yameandaliwa Igo Africa for Jesus na Makanisa na Huduma za Tanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: