Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale akiwa katika picha ya pamoja na watafiti toka COSTECH na maafisa ugano 53 wa wilaya hiyo.

Mkuu wa wilaya ya Nyang'wale Hamimu Gwiyama akifungua Mafnuzo hayo ya siku Moja.

Mtaribu wa OFAB Tanzania, Philbert Nyinondi akizungumza na wagani lengo ya mafunzo hayo.

Na Mwandishi Wetu.

Wito Umetolewa kwa Maafisa Ugani waliopo katika Wilaya ya Nyang’wale Mkoani Geita kutumia nafasi zao vizuri katika kwa wakulima ili kuwafanya kulima kilimo cha kisasa ambacho kina tija katika Jamii kwa ujumla.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa wilaya ya Nyang’wale Hamimu Gwiyama wakati akifungua mafunzo kwa maafisa Ugani 27 kutoka wilaya hiyo yaliyoandaliwa na Tume ya taifa ya sayansi na teknolojia COSTECH kupitia Jukwaa la bioteknolojia la Kilimo(OFAB) yenye lengo la kuwakumbusha wataalamu hao nafasi yao katika kilimo ili kutoa mbinu kwa wakulima kuwa na kilimo cha kisasa hasa katika mazao ya mizizi.

Mh Hamimu alisema kwamba kuna fursa nyingi katika Mkoa huo hasa zinazo husu kilimo kama wagani hao wataweza kufanyia kazi ipasavyo mafunzo hayo watakayo pewa na wataalamu basi wakulima wataanza kuneemeka.

“Zipo fursa nyingi katika wilaya hiyo ambapo upo uwezekano wa kulima mazo ya Pamba,Dengu,Mahindi kama mafunzo hayo mtafanyia kazi vizuri naamini njaa katika wilaya yangu ni historia”Alisema Hamimu

Kwa upande wake Mratibu wa OFAB Tanzania Philbert Nyinondi alisema wapo katika kutekeleza sera ya nchi ya uchumi wa viwanda hivyo wameona ni vyema kutoa elimu namna ya kupata kilimo cha kisasa na chenye tija ambacho kitainua pato la Taifa.

“Kikubwa kilichotuleta ni kuweka makundi haya makubwa mawili kati ya wagani na watafiti ili kwa pamoja waweze kujua namna ya kutataua changamoto ya kilimo ili kwenda katika uchumi wa viwanda” Alisema Nyinondi

Hata hivyo baadhi wa wagani katika wilaya hiyo wamesifu mafunzo hayo na kusema kwamba fursa za kilimo zilizopo katika wilaya hiyo zitaenda vizuri kama bajeti wakitengewa na kuweza kuwa na mashamba darasa kwa wakulima ambapo itakuwa rahisi kwao kutoa elimu vizuri kwa wakulima.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: