Mtendaji Mkuu Wa Benki Ya Tpb, Sabasaba Moshingi (Wa Pili Kushoto) Na Kaimu Mkurugenzi Wa Mfuko Wa Jamii Zanzibar (Zssf) Makame Mwadini Wakitiliana Saini Makubaliano Ya Kutoa Mikopo Ya Kielimu Na Kuazia Maisha Kwa Wanachama Wa Zssf, Hafla Hiyo Imefanyika Katika Ukumbi Wa Zssf Kilimani Mjini Zanzibar. Wakishuhudia Tukio Hilo Ni Afisa Mawasiliano Wa Benki Ya Tpb Bi. Chichi Banda (Kushoto) Na Afisa Wa Sheria Wa Zssf Bw. Fadhil Mohammed (Kulia).
Afisa Mtendaji Mkuu Wa Benki Ya Tpb Bw. Sabasaba Moshingi (Wa Tatu Kushoto) Na Kaimu Mkurugenzi Wa Mfuko Wa Jamii Zanzibar (Zssf) Makame Mwadini Wakikabidhiano Mikataba Ya Utoaji Mikopo Ya Kielimu Na Kuanzia Maisha Kwa Wanachama Wa Zssf, Hafla Hiyo Imefanyika Katika Ukumbi Wa Zssf Kilimani Mjini Zanzibar. Wakishuhudia Tukio Hilo Ni Wakurugenzi Na Maofisa Kutoka Benki Ya Tpb Na Mfuko Wa Hidhafi Ya Jamii Zssf.
Makabidhiano Ya Mkataba Wa Makubaliano Baina Ya Benki Ya Tpb Na Zssf.
---
BENKI ya TPB imetiliana saini na Mfuko wa Hifadhi Zanzibar (ZSSF), kwa ajili ya mkopo wa kujikimu na wa elimu ya juu kwa wananchama wa mfuko huo. Utiaji wa saini ulifanyika jana na kwa upande wa TPB, Afisa Mtendaji Mkuu, Sabasaba Moshingi aliiwakilisha benki yake na kwa ZSSF iliwakilishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Mfuko huo, Makame Mwadini Silima.

Akizungumza mara baada ya utiaji wa saini hiyo Moshingi, alisema huduma hiyo muhimu kwa wafanyakazi ambao wanaanza maisha na wale ambao wanataka kuongeza elimu na kuwataka wanachama wa Mfuko huo kuchangamkia fursa ya mikopo ili kujiendeleza kimaisha.

Alisema kuwa benki yao itakuwa ikitoa mikopo kwa wanachama hao na baada ya muda watakuwa wakirjesha kwenye mishahara yao.

Alisema kuwa katika huduma hiyo kila atakayekopa atakaywa riba ya asilimia 12 ya mkopo wake ambayo aliielezea ni ndogo kulingana na aina ya riba ya mikopo mengine.

Alisema kuwa huduma hii ya mkopo wa kujikimu na wa elimu ya juu imeanza Dar es Salaam kupitia Mfuko wa Pensheni wa PSPF pamoja na GEPF na jana ZSSF walitiliana mkataba baada ya kuona umuhimu wa kuwasaidia wanachama wao.

Kaimu Mkurugenzi wa ZSSF, Mwadini alisema kuwa hatua hiyo mbali ya kuwawezesha wananchama wao, itawasaidia kuongeza wanachama wapya kwa sasa wana wanachama zaidi ya 70,000.

Alisema kuwa wamefanya mambo mbalimbali ikiwamo kukabiliana na changamoto za wanachama wao na kuboresha ustawi wa Wazanzibari na Watanzania.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: