Mkuu wa Wilaya ya NZEGA Godfrey Ngulupa akifungua Mafunzo ya Maafisa ugani Nzega.

Hadija Kaboyela.
Mratibu wa Ofab Tanzania Philbert Nyinondi akitoa Maelezo kwa Mkuu wa wilaya pembeni yake ni waandishi wa habari.
Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa wilaya ya Nzega na Maafisa Ugani wa wilaya ya Nzega.

Na Helen Isdory.

Mkuu wa Wilaya Nzega Godfrey Ngupula amewataka wanasiasa pamoja na wanaharakati kuacha kupinga kila tafiti za wanasayansi kwa Maneno badala yake wapinge tafiti kwa kutoa nao tafiti ili kuepuka kutoa mkanganyiko wa uelewa kwa wananchi.

Hayo alibainishwa na Mkuu wa wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula wakati akifungua Mkutano wa maafisa ugani 63 katika wilaya hiyo,Mafunzo yaliyoandaliwa na Tume ya sayansi na Teknolojia (COSTECH) kupitia Jukwaa la bioteknolojia kwa Maendeleo ya Kilimo(OFAB) yenye lengo la kuwakumbusha wagani hao namna ya kutumia kilimo cha kisasa chenye manufaa kwa Jamii.

Mhe. Ngulupa alisema kwamba ipo haja kwa wanasiasa kuwa na siasa safi na siziso kuwa na athari kwa jamii hususani kuweka vipingamizi katika tafiti za wanasayansi jambo ambalo linaweza kuleta athari kwa jmaii ikiwa sasa kuna uhitaji Zaidi teknolojia mbalimbali hususani katika sekta kilimo ambapo Mabadiliko ya hali ya hewa yana athiri sekta hiyo pia

“Mwalimu nyerere alisema mambo yamisingi ambayo Jamii inatakiwa kjua kuwa na siasa safi tuache siasa za maji taka ambapo kitu cha kisayansi kinapingwa kwa Tafiti za kisayansi na si kupinga bilia kuja wanachopinga,Hivyo wanansiasa wanatakiwa kuwasilikila wanasayansi na kuelewa wanachosema kwani wanawajibu ya kuleta utafiti katika jamii ambapo baada ya wao inatakiwa watunga sera kuangalia Tafiti zao na kuzifanyia kazi na si kila mwanasiasa kupinga Tafiti za kisayansi kwa Maneno”

Aidha Mhe. Ngulupa alisema kuwa kwasasa anajitahidi sana wananchi wake waweze kupata mazao ya chakula ili waweze kuepeukana na njaa hivyo wana uhitaji mkubwa wa mbegu ambazo zitaendana na hali ya hewa ya sasa.

“Mimi ni mwanasiasa na kiongozi wa wilaya lakini najua kabisa wananchi wakiwa na njaa siwezi kuwaongoza ila mwenye njaa dawa yake si siasa sasa kutokana na mabadadiliko ya hali ya hewa hapa wilayani wananchi wangu nimewasisistiza kulima mihogo,Viazi vitamu,Mtama pamoja na pamba ili kupata hela sasa mlipokuja na kunieleza kuwa kuna mbegu za Mihogo zenye kuhimili magonjwa pamoja na mbegu za mahindi za wema ambazo ni mimi nilikuwa natamani kama ningezipata hizo mbegu hapa katika wilaya yangu ilikuanza kutumia”

Hata hivyo wilaya ya nzega imesemekana bado ipo katika hali ya mbaya ya kilimo kutokana na hali ya hewa hivyo kwasasa wanatumia kilimo cha mihogo tu katika kujipatia kipato na chakula jambo ambalo lina athari kwa Jamii.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: