Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu NchembaMaliyevaa suti nyeusi akisalimiana na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege Mjini Dodoma, kwa ajili ya kufungua Kikao cha Makamanda wa Jeshi hilo mapema leo asubuhi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akiangalia kikundi cha ngoma mara baada ya kuwasili uwanjani hapo mapema leo asubuhi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye wapili toka kulia, Kamishna wa Utawala na Fedha Michael Shija na Kamishna wa Utawala na Rasilimali watu Billy Mwakatage wakiimba wimbo wa Taifa mara baada ya kuingia kwenye ukumbi wa Mikutano wa LAPF kinapofanyika Kikao cha
Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye akisoma hotuba ya kumkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba katika Kikao cha Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akisoma hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Makamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mapema leo asubuhi.
Sehemu ya Makamanda wa Mikoa wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi mapema leo asubuhi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akiwa katika picha ya pamoja na Kamishna Jenerali Thobias Andengenye, Makamishna Waandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Dodoma (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: