Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

Bodi ya wadhamini ya Soka Simba sports klab imedhamiria kuwapeleka mahakamani viongozi wa club hiyo endapo wataitisha mkutano unaotarajia kufanyika mnamo Agosti 13 na 23 mwaka huu.

Ameyasema hayo mwenyekiti wa wa baraza la wazee Simba Hamis Kilomoni leo Nyumbani kwake jijini Dar es salaam,Alisema kuwa kikao kihairishwe mpaka watakapotoa tamko la mahakamani juu ya viongozi hao wa klabu hiyo.

Kilomoni amesema kuwa Timu ya Simba sio masikini kama vile watu wanavyofikiria,"Leo hii tujiulize mbona timu imeenda Afrika Kusini imejadiliwa na nani na je imejadiliwa na mkutano mkuu" Amesema mzee Kilomi.

Nae katibu wa bodi ya udhamini Simba Danke Nkwabi amesema kuwa umoja ni nguvu hivyo wadhamini wa simba waungane wawe kitu kimoja katika kuijenga klabu hiyo na kuvunja utengano uliopo kati ya Simba halisi na Simba wahindi.

Hata hvyo mwanachama wa Simba Kipepa Kasim amesema huku wakisubiri tamko la mahakama viongozi walioteuliwa kwa muda waendelee na maandalizi yao ya Simba day.

Sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika Agosti 8 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam ambao Watafuana na Rayon Sports kutoka Nchini Rwanda.Ikiwa siku hiyo itakuwa ni utambulisho rasmi kwa wachezaji wapya waliosajiliwa msimu huu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: