William Henry Gates III maarufu kama Bill Gates na Mwanzilishi wa kampuni ya Microsoft iliyomfanya kuwa mtu tajiri namba moja duniani na mwanzilishi wa mashirika lukuki yasiyo ya kiserikali yenye kusaidia jamii yupo nchini Tanzania.

Jana Agosti 9, 2017 ametembelea kijiji cha Kicheba wilayani Muheza katika mkoa wa Tanga kwa lengo la kujifunza jinsi zoezi la ugawaji dawa za matende na mabusha zinavyofanyika nchini ikiwa ni jitihada za kutokomeza magonjwa yasilokuwa hayapewi kipaumbele nchini. Ikiwa ni pamoja na kuangalia ni namna gani anaweza kusaidia kwenye sekta hiyo ya Afya.
Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo akimkaribisha Bilionea Bill Gates mara baada ya kutembela kijiji cha Kicheba, Muheza - Tanga.
Bilionea Bill Gates akitoa shukrani zake kwa mapokezi aliyoyapata.
Mbunge Mhe. Adadi Rajabu akitoa machache mbele ya kikao na Bilionea Bill Gates wakati alipotembela katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga jana Agosti 9, 2017.
Bilionea Bill Gates akisalimiana na viongozi wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, mara baada ya kutembelea wilaya hiyo katika kijiji cha Kicheba jana Agosti 9, 2017.
Mmoja ya viongozi akitoa maelezo machache kwa mgeni wao Bilione Bill Gates alipotembelea kijiji cha Kicheba, wilayani Muheza, Tanga jana Agosti 9, 2017.
(kushoto) akiwa na Bill Gatesbpamoja na mmoja wa viongozi wa kinamama wa wilaya hiyo katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga jana Agosti 9, 2017.
Bill Gates akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa wilaya ya Muheza akiwamo Mkuu wa Wilaya Mkuu wa wilaya ya Muheza Mkoani Tanga, Mhandisi, Hajat Mwanasha Tumbo na Mbunge Mhe. Adadi Rajabu (wa nne kulia) katika kata ya Kicheba Wilayani humo mkoani Tanga jana Agosti 9, 2017.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: