Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai leo ametembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu na kufanya mazungumzo na Spika mwenzake, Dr Amal Al Qubaisi ambapo amewasilisha mapendekezo rasmi ya kuanzisha Umoja na Urafiki wa Kibunge baina ya Bunge la Tanzania na Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu.

Mhe Spika Al Qubaisi ambae ni Spika wa kwanza mwanamke katika nchi zote za Mashariki ya Kati kwa niaba ya Bunge la nchi hiyo amekubali mapendekezo hayo na kutoa mwaliko Kwa Wabunge wa Tanzania kutembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu kwa nia ya kuona namna UAE ilivyopiga hatua.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akisaini kitabu cha wageni alipotembelea Bunge la Umoja wa Falme za Kiarabu, Abu Dhabi. kulia kwake ni Spika wa Bunge hilo, Dr Amal Al Qubaisi.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akiwa na mwenyeji wake, Dr Amal Al Qubaisi baada kuzungumza nae.
Spika Job Ndugai akipewa ziara ya Bunge la nchi hiyo na Spika Al Qubaisi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: