Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane kanda ya kaskazini Arusha, akaeleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu(Habari picha na Pamela Mollel Arusha).
Afisa Masoko wa kampuni ya ALAF jijini Arusha Finias Wanguba akionyesha bati aina yaTekdek inayozalishwa na kampuni hiyo jijini Arusha.
Meneja mauzo kanda ya kaskazini Edward William akionyesha aina ya mabati yanayopatikana katika kampuni yao
Wateja wakiwa katika banda la kampuni ya ALAFwakipewa maelezo juu ya ubora wa bidhaa hiyo
Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali

Na Pamela Mollel, Arusha.

Kampuni ya ALAF inayozalisha na kusambaza mabati ya aina mbalimbali ya rangi pamoja na bati maarufu simba dumu imekuwa ikihudumia watanzania kwa zaidi ya miaka 50

Akizungumza katika maonyesho ya nanenane kanda ya kaskazini Afisa Mauzo wa kamapuni ya ALAF Finias Wanguba alisema kuwa mabati hayo yana ubora wa hali ya juu na bei zake ni za kawaida tu hivyo mwananchi yeyote anaweza kumudu kununua.

Pia katika maonyesho hayo ya nanenane kamapuni hiyo imetoa punguzo la bei katika bidhaa zake.

Mabati haya hupatikana kanda ya kaskazini Arusha, kanda ya kati Dodoma,kanda ya ziwa Mwanza,Nyanda za juu kusini Mbeya, Dar es Saalam.

Hata hivyo kiwanda cha ALAF ni kiwanda cha kwanza Tanzania kilicholeta teknologia ya bati la msauzi ambapo huzalisha bati na chuma.

Kwa upande wake Mteja kutoka Simanjiro alipata fursa ya kutembelea banda la ALAF katika maonyesho ya nane nane Mkoa Arusha, alieleza ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kampuni ya ALAF ambapo amewataka watanzania kupenda na kuthamini bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa kuwa zinaubora wa hali ya juu.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: