Thursday, August 3, 2017

KATIBU MKUU WIZARA YA KILIMO ATEMBELEA BANDA LA COSTECH VIWANJA VYA NANENANE NGONGO MKOANI LINDI

Mtafiti kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Bestina Daniel (kushoto), akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mathew Mtigumwe (kulia), kuhusu ushiriki wa COSTECH katika maonyesho hayo, alipotembelea banda la COSTECH, lililopo chini ya Wizara hiyo katika Maonyesho ya Kitaifa ya Wakulima yanayoendelea Viwanja vya Nane Nane vya Ngongo mkoani Lindi jana.
Mtafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Mikocheni (MARI), Ismail Ngolinda, akitoa maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mhandisi Mathew Mtigumwe (kushoto), alipotembelea banda hilo. Katikati ni Mkurugenzi wa Utafiti na Maendeleo wa Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi, Hussein Mansour.
Watafiti wakijadiliana jambo kwenye maonesho hayo. Kutoka kulia ni Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB), Filbert Nyinondi, Bestina Daniel, mdau wa kilimo, Flaviana, Dk. Emmarold Mneney, Ismail Ngolinda kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo cha Ilonga Kilosa mkoani Morogoro na Christina Kidulile.
Taswira ya banda hilo katika maonyesho hayo.

No comments :

Truck Driving Schools
Idadi ya Watu