Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati), akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Tanzania, Bw. Le Van Dai (kulia) wakati wakisaini mkataba wa kusambaza mawasiliano ya simu kwa kujenga miundombinu maeneo ya vijijini, chini ya Mradi wa sita wa kufikisha mawasiliano kwa wote, kwenye makao makuu ya UCSAF barabara ya Bagamoyo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam Agosti 18, 2017. UCSAFimesaini makubaliano kama hayo na makampuni mengine ya simu hapa nchini ikiwemo, Vodacom Tanzania PLC, Airtel, tigo na TTCL.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MFUKO wa Mawasiliano Kwa Wote Nchini, (UCSAF), umesaini mkataba na makampuni matano ya simu hapa nchini wa utekelezaji wa Mradi wa Sita wa Kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote.

Mikataba hiyo imesainiwa mbele ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Manyaa Mbarawa.

Makampuni yaliyotia saini mkataba huo ambao utayawezesha, kujenga miundombinu ya kupeperusha mawasiliano ya simu kwenye mmbalimbali hususan vijijini ni pamoja na Halotel, Airtel, Vodacom Tanzania PLC, TTCL na TIGO.

Waziri Profesa Mbarawa alishuhudia Afisa Mtendaji Mkuu wa UCSAF kwa niaba ya Mfuko, akisaini mikataba hiyo na Maafisa Watendaji Wakuu wa makampuni hayo mbele ya waandishi wa habari.

Kwa mujibu wa maafisa wa UCASAF, kusainiwa kwa mikataba hiyo ni moja ya kutekekeleza malengo makuu ya Mfuko ambayo ni pamoja na kuhakikisha upatikanaji wa huduma ya mawasiliano katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu.

Lakini pia ni kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi na serikali katika utoaji wa huduma za mawasiliano kwa wote katika maeneo ya vijijini yenye mawasiliano hafifu.

Malengo mengine ni pamoja na Kuhamasisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi katika maeneo ya vijijini na maeneo ya mijini yenye mawasiliano hafifu;

Kutengeneza mfumo kwa ajili ya upatikanaji wa mitandao ya mawasiliano na huduma rahisi na zenye ufanisi katika uzalishaji na upatikanaji katika soko la kiushindani;

Maafisa hao wamesema lengo linguine ni kuhamasisha utoaji wa huduma bora katika viwango nafuu na kuhakikisha kuwa teknolojia ya habari na mawasilianpo inapatikana vijijini na sehemu za mijini zenye mawasiliano hafifu kwa bei nafuu.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, amewahakikishia wawekezaji ushirikiano uklio dhahiri kutoka serikalini na kuwataka, waongeze kasi ya uboreshaji wa mawasliano ya simu ili wananchi hususan wa vijijiniwaweze kutumia teknolojia ya mawasiliano kuharakisha maendeleo yao.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, akitoa hotuba yake
Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw. Joseph Kilongola, akizungumza kwabla ya kumkaribisha Profesa Mbarawa kutoa hotuba
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, akielezea lengo la kusainiwa kwa mikataba hiyo ya utekelezaji wa Mradiwa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote.
Baadhi ya maafisa wa makampuni ya simu na UCSAF.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Suingano Malya, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba wa sita wa kepeleka mawasiliano ya simu kwa wote.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, (kulia), akimpongeza Mwakilsh wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya, mara baada ya Airtel kusaini mkataba wa sita wa Mradi wa kupeleka mawasiliano ya simu kwa wote na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, (UCAF), jijini Dar es Salaam, Agosti 18, 2017.
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Airtel, Bi. Beatrice Singano Malya wakisaini mkataba wa Mradi wa sita wa kupeleka mawasiliano kwa wote.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Bw. Ian Ferrao, wakibadilishana hati baada ya kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, wakisaini mkataba huo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, wakibadilishana hati baada ya
kusaini mkataba utakaowezesha kusambaza Mawasiliano kwa wote hususani vijijini. UCSAF imesaini makubaliano na makampuni yote ya simu nchini kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya Mfuko huo jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mnyaa Mbarawa(katikati)akiwashuhudia Afisa Mtendaji Mkuu (CEO), wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Mhandisi. Peter Ulanga, (kushoto), na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Mhandisi Cecil Nkomola Francis, wakisaini mkataba huo.
Mhandisi Ulanga, akimpongeza Bw. Ferrao wa Vodacom.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TIGO, Bw. Simon Karikari, akiwa miongoni mwa maafisa wenzake wakisikiliza hotuba ya Mhe. Waziri
Profesa Mbarawa, akipena mikono na Mwenyekiti wa Bodi ya UCSAF, Bw.Joseph Kilongola.
Wakuu wa makampuni ya simu za mikononi nchini.
Bw. Ferrao, akitoa hotuba ya shukrani kwa niaba ya wenzake
Profesa Mbarawa na Mhandisi Ulanga, wakionyeshana kitu
Baadhi ya maafisa wa makampuni simu na UCSAF.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: