Bi. Rehema uvimbe unavyoonekana.
Akiwa nje ya hospitali ya KCMC.
Akiwa ameshapatiwa kitanda Katika hospitali ya Taifa Muhimbili

Na Vero Ignatus Arusha.

Hatimae Rehema Juma Kishena (40) aliyekuwa anaomba msaada wa matibabu kutokana na uvimbe unaomsumbua kwa miaka 17 amefanikiwa kwenda hospitalini kwaajili ya matibabu

Bi. Rehema kupitia msaada wa wasamaria wema walioweza kumsaidia kwa kiwango cha fedha kidogo tarehe 22/8/2017 alifanikiwa kwenda hospitali ya KCMC akampatia rufaa kuelekea Muhimbili tokea tarehe 28/8/2017

Akizungumza na mwandishi wa blog hii dada wa Mgonjwa Aziza Bakari Muyai amesema kuwa tayari siku ya leo wamefika hospitali ya Muhimbili wanatarajia majibu kutoka kwa madaktari watakaomuhudumia mgojwa ili waelewe hatua itakayofuata.

Aidha Bi Aziza amewashukuru wale wote waliomsaidia hadi mdogo wake Kuanza matibabu, amewaomba wasichoke kwani hali ya mgonjwa bado haijatengamaa.

Bi Rehema Juma Kishena (40) amelazwa Katika hospitali ya Muhimbili Jengo la Sewa Haji, Wodi namba 24 Kitanda namba 16.

Uongozi wa Blog hii unatoa shukrani kwa Wale wote waliosoma habari kuhusiana na tatizo linalomsumbua Rehema kupekekea kuomba msaada wa matibabu, tunawashukuru wale wote waliojitoa kwa hali na mali ili kuhakikisha kuwa Bi Rehema anapatiwa matibabu Mungu awazidishie kila mlipotoa.

Ameomba kwa yeyote aliyepo tayari kumsaidia atumie mawasiliano kwa namba 0653179373
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: