Jina lake halisi anaitwa N!xau. Inakadiriwa alizaliwa kati ya mwaka 1943 au 1944, kwani yeye binafsi hakuwa akijua umri wake. Alikuwa ni mzaliwa wa nchini Namibia kijiji cha Tsumkwekatika jangwa la Kalahari.

Hakuwahi kujifunza sanaa ya uigizaji hapo kabla, kwa sababu huyu alikuwa ni mtu pori halisi (yaani kama vile anavyoishi kwenye muvi zake basi huo ndio uhalisia wa maisha yake aliyokuwa akiishi hapo kabla) hivyo katika maisha ya porini na Jangwani hakukuwa na sanaa ya maigizo.

Ila wazungu walimtafuta mtu ambaye alikuwa ni bushman halisi ili wamuweke kwenye muvi zao ndipo wakakutana na huyu bwana.

Hivyo alianza maisha yake mapya ya ucheza filamu mwaka 1980 -1994. Zifuatazo ni filamu maarufu zaidi alizopata kucheza na zikaja kuwa kubwa Zaidi ulimwenguni kote hata kufanikiwa kujishindia TUZO mbalimbali:

"The Gods Must Be Crazy II, Crazy Safari, Crazy Hong Kong na The Gods Must Be Funny in China".

Katika movie yake ya kwanza ambayo ni "The Gods Must Be Crazy "alilipwa dollars 300 tu za kimarekani, ambazo kiuhalisia ni kiasi kidogo mno cha pesa, lakini hela hizo zote alizichana sababu hakuwa akijua matumizi ya hela kwa sababu hapo awali hakuwa kutumia hela. Ila baadae baadae alifundishwa umuhimu wa hela, hivyo katika filamu zilizofuata akaanza kudai malipo tena makubwa kweli kweli.

Pia kabla ya kucheza filamu yake ya kwanza alikuwa bado hajawahi kuwaona Wazungu machoni pake, tena hakuwa amewahi kufika mjini.

Baada ya kumaliza maisha yake ya uigizaji huko ughaibuni ndipo aliporudi nchini kwao Namibia, ndipo alipoanza maisha mapya alijenga nyumba nzuri ya kifahari kisha akaanza kujihusisha kwa shughuli za kilimo na ufugaji, ambapo katika mifugo aliyokuwa akifuga haikuzidi idadi ya 20, na hiyo ni kwa sababu hakuwa akiweza kuhesabu zaidi ya 20. Lakini bado hakuacha tamaduni yao ya Uwindaji hivyo aliendelea kuwa hivyo licha ya utajiri aliokuwa nao.

Nchini kwao Namibia anaheshimika mno kuwa ndiye Msanii mkubwa na mtu maarufu zaidi kuwahi kutokea nchini mwao.

Hapo kabla hakuwa na dini hivyo mwaka 2000 ndipo alipoamua kubatizwa na kuwa msabato. Hatimaye tarehe 1 July 2003, alifariki baada ya kuugua kifua kikuu kilichokomaa ugonjwa alioupata kutokana na baridi ya uwindaji wa ndege usiku. Anakadiriwa kufa akiwa na miaka 59 baada ya kufariki alizikwa kwenye makaburi ya asili huko Tsumkwe mnamo 12 july 2003 pembeni mwa kaburi la mke wake wa pili, aliacha watoto 6.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: