Balozi wa Mchezo wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kushoto), akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 30 mshindi wa droo ya Jumapili ya Jackpot ya Tatu Mzuka, Tausi Mashombo jijini Dar es Salaam jana, aliyojishindia kutoka katika mchezo wa Tatu Mzuka ambao umejizolea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea Jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.
Mshindi wa milioni 30 ya droo ya Jumapili ya Jackpot ya Tatu Mzuka, Tausi Mashombo, wa pili kushoto, akiwa na marafiki zake ambao wote wamejishindia milioni 1 kwenye kampeni ya Cheza na Shinda na Marafiki. Kutoka kulia ni Riwa Lyimo akifuatiwa na Edna Msangi. Tatu Mzuka ambao wanaendesha droo ya kila saa na washindi kuweza kujishindia hadi shilingi milioni 6, sasa wanaendesha droo ya Shinda na Marafiki, ambapo pia inatoa fursa kwa washiriki watatu kushinda shilingi milioni moja kila mmoja.
Mshindi huyo, Tausi Mashombo akionyesha alama ya tatu mzuka mara baada ya kukabidhiwa zawadi yake.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: