Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, wakati alipotembelea vitengo mbalimbali vya shirika hilo, kuongoea na Uongozi pamoja na wafanyakazi, Dar es Salaam leo. Wa tatu ni Kaimu Katibu wa Shirika, Zuhura Pinde. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akipatiwa maelezo na Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo kuhusu utendaji kazi wa kitengo cha utumaji na upokeaji wa fedha cha Western Union, katika ziara hiyo.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo (kulia), akimpatia maelezo Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani kuhusu idara mbalimbali za Posta Kuu, wakati alipotembelea sehemu hiyo katika ziara hiyo. Kushoto ni Meneja wa Posta, Mkoa wa Dar es Salaam, Margret Mlyomi.
Kaimu Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo, akizungumza wakati akimkaribisha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kushoto kwake), kuzungumza na Uongozi wa shirika hilo, wakati wa ziara hiyo. Kulia ni Meneja Mkuu Uendeshaji wa shirika, Hassan Mwang'ombe.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (katikati), akizungumza na uongozi wa Shirika la Posta katika ziara hiyo.
Baadhi ya viongozi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipokuwa akizungumza nao leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano wao na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani, alipofika kwenye taasisi hiyo, kukagua sehemu mbalimbali za shirika, kuzungumza na Uongozi pamoja na wafanyakazi.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: