Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli  akichukua Tiketi zake pamoja na chenchi mara baada ya kulipia huduma ya  Kivuko wakati akielekea katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere  Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana pamoja na kuzungumza na abiria mbalimbali wakati akisubiri
kuvuka kwa kutumia usafiri wa Pantoni kuelekea katika Chuo cha
Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akimsikiliza Yusuph Ndemango ambaye ni mlemavu wakati alipomkuta ndani
ya jengo la abiria lililopo upande wa Magogoni kabla ya kuvuka na
Pantoni kuelekea  katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere
Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiingia katika kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine  wakati
akivuka kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
ndani ya Kivuko cha MV Kigamboni pamoja na abiria wengine wakati akivuka
kuelekea upande wa pili wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasili upande wa Kigamboni mara baada ya kushuka pamoja na abiria
wengine kwenye pantoni la MV Kigamboni.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Mama mmoja mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni
jijini Dar es Salaam.
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akinunua chapati mara baada ya kuvuka upande wa Kigamboni wakati wa
asubuhi.
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akiwasalimia wakazi wa Kigamboni mara baada ya kuvuka kwa kutumia
usafiri wa Pantoni wakati katika Chuo cha Kumbukumbu ya  Mwalimu Nyerere
Kigamboni  jijini Dar es Salaam. 
 Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa
katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Minazini
Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akiimba pamoja na wanachama wa CCM waliopo katika kambi
ya mafunzo ya vijana iliyoandaliwa na Umoja wa vijana wa vyuo na Vyuo
vikuu(CCM) katika Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es
Salaam.
 Wanachama hao wakiimba mara baada ya Mwenyekiti wa CCM Taifa kuwasili ukumbini hapo.
 Mwenyekiti
wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na wanachama wa CCM waliopo katika kambi ya
mafunzo ya vijana iliyoandaliwa na Umoja wa vijana wa vyuo na Vyuo
vikuu(CCM) katika ukumbi wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere
jijini Dar es Salaam.

 PICHA NA IKULU
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: