Mkurugenzi wa Mifumo ya Tehama kwenye mradi wa PS3 Desderia Wengaa akitoa maelezo ya Utangulizi wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya Planrep na FFARS.
Baadhi ya washiriki kutoka Mikoa mitano ya Tanga, Tabora, Manyara, Singida na Dodoma wakati wa mafunzo ya Planrep na FFARS.
Erick Kitali Mkurugenzi wa TEHAMA, OR-TAMISEMI akielezea kwa ufupi mifumo iliyoboreshwa ya Planrep na FFARS wakati wa mafunzo yanaendelea Mkoani Dodoma.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Dododma Rehema Madenge akifungua mafunzo ya siku nane kwa wataalamu wa Afya, Mipango na Fedha kutoka Mikoa Mitano chini ya ufadhili wa mradi wa Uimarishaji Mifumo (PS3).
Pichani ni Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge (Katikati mbele) akiwa na wakufunzi wa mafunzo hayo.(Picha zote na Ofisi ya Rais TAMISEMI)
---
Serikali mkoani hapa imesema ili mpango wa PlanRep uweze kufanikiwa kwa ufasaha hakuna budi kuzijumuisha idara za Elimu katika mafunzo yanayoendelea mkoani Dodoma yanayo wajumuisha wataalam wa mipango pamoja na afya kutoka mikoa mitano ya Tanga, Tabora, Manyara, Singida na wenyeji Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya bajeti kwakutumia mfumo mpya wa PlanRep na FFARS.

Akifungua mafunzo ya siku nane mkoani hapa, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Bibi Rehema Madenge, amesema moja ya vitu vilivyokuwa vikikwamisha masuala ya bajeti ni pamoja na kutokuwa na takwimu sahihi huku akinyooshea kidole takwimu za idara za elimu.

“Ninatamani sana takwimu za elimu ziwe sahihi hasa katika uwasilishaji wa taarifa za mitihani ili ziweze kuendana na idadi ya wanafunzi na fedha zinazo ombwa, kuepusha madudu yanayo wasilishwa” alisema madange na kuongeza kuwa katika sekta ya elimu ndipo kuna sarakasi ambazo hata mruka sarakasi mwenyewe hata yeye hamjui.

Madenge ambaye kwa taaluma ni Mchumi na aliyeshughulika na kuratibu shughuli za bajeti kwa muda mrefu, amesema ili mipango iweze kuendana na mahitaji suala la kuwa na takwimu sahihi haliepukiki na kuamini kuwa chini ya PlanRep mpya itakuwa mwarobaini katika kutatua changamoto hizo.

Madenge amesema mfumo wa PlanRep ulioboreshwa pia unaenda kutumika kuanzia ngazi ya msingi yaani vituo vyetu vya kutolea huduma ambapo utawezesha kuandaa mipango na bajeti kutokana na vipaumbele na mahitaji ya wananchi ambao ndio waathirika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa mifumo ya TEHAMA wa PS3, Desderi Wangaa, amesema, PlanRep mpya iliyoboreshwa imefanyia kazi changamoto kwa kuhakikisha kwamba mipango na bajeti unaingizwa kwa kila mtoa huduma, na unaingiza namba za utambulisho kwa kila mtoa huduma mmoja mmoja kwa kila sekta lakini pia mfumo huu umeweka nafasi ya kila mtoa huduma kuainisha matokeo yanayotegemewa (Service Outputs).

Awali akitoa maelezo ya utangulizi, Mkurugenzi wa TEHAMA wa OR-TAMISEMI, Erick Kitali, alisema mfumo umezingatia mahitaji ya idara zote za mamlaka za serikali za mitaa na ambao ni fungamanifu unaotumia muda mfupi kukamilisha kazi za uratibu wa bajeti na taarifa za hesabu toka vituo vya huduma.

“Kutokana na kuwa fungamanifu hatutegemei kuona Serikali za Mitaa zikikwama katika uandaaji wa bajeti, na tuna uhakika na ufanisi wa hali ya juu katika kazi hii usahihi unaotakiwa” alisema Erick na kuongeza (Efficient and Effective).

Awali akimkaribisha Katibu Tawala wa Mkoa, Mkurugenzi wa mamalaka za serikali za Mitaa Beatrice Kimoleta, alisema kuwa na mfumo ni jambo moja na utendaji ni suala linguine hivyo suala la kujituma katika kuhakikisha mifumo inafanya kazi vema kila mmoja lazima awiwe katika utendaji wake.

“Tulitumia muda mwingi katika kuandaa bajeti na muda mfupi ukatumika katika kusimamia lakini katika PlanRep hii mpya mtaona muda wa uandaaji bajeti utakuwa utakuwa mfupi na muda mwingi utatumika katika suala la ufatiliaji na usimamizi”. Rai yangu niwasihi sote tuwe makini wakati wote wa mafunzo ili tukitoka hapa basi mipango yetu iwe yenye kuzingatia mahitaji.

PS3 kwakushirikiana na OR-TAMISEMI tayari wametoa mafunzo kwa mikoa na Halmashauri zote nchini na katika awamu hii ya mwisho inahusisha wataalamu kutoka mikoa ya Tanga, Tabora, Singida Manyara na Dodoma ambayo ni mwenyeji.

Aidha uzinduzi wa PlanRep mpya utafanyika 5 Septemba, 2017 na Mgeni Rasmi anatazamiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassimu Majaliwa (MB).
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: