Msimamizi wa Zoezi la pamoja kwa vikosi maalumu vya Majeshi ya SADC ambalo limepewa jina la Matumbawe, Meja Generali Harison Msebu katika kupambana na matishio mbalimbali ya usalama kushoto akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kuanza zoezi hilo ambalo litaanza Agosti 2 hadi Septemba 1 Jijini Tanga,kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigella.
---
VIKOSI vya Majeshi ya Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwaafrika (SADC SPECIAL FORECES) vimeamua kupambana na ugaidi,Uharamia kwa kushirikiana kufanya zoezi la pamoja
lililopewa jina la “EX MATUMBAWE” ikiwa ni mkakati wa kutokomeza vitendo hivyo.

Zoezi hilo litakaloshirikisha vikosi vya Makomandoo, Ndege za kivita,meli za kivita na makomandoo watakao ruka na miavuli huku wote kwa pamoja kutoka nchi zote shiriki watafanya mazoezi hayo kubadilishana uzoefu litafanyika kuanzia Agosti 2 mpaka Septemba 1 mwaka huu katika maeneo ya Mapango ya Mleni.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Tanga,Msimamizi wa Mazoezi hayo, Meja Generali Harison Msebu alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni kufanya mazoezi ya pamoja kwa vikosi maalumu vya Majeshi ya SADC,ili kuviwezesha kuwa na utayari na harakati katika kupambana na matishio mbalimbali ya usalama.

Aidha alisema kuwa kutasaidia kuviwezesha vikosi hivyo kukabiliana na masuala ya Ugaidi,Uharamia na maafa yatokanayo na mabadiliko ya hali ya hewa na kusaidia vikundi vya kulinda amani kama ilivyoelekezwa na Jumuiya ya SADC pamoja na umoja wa Afrika (AU).

Alisema Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Mwaafrika zimejiwekea mikakati ya kuondoa uhasama wao na zaidi kuunganisha mahusiano ikiwa na
lengo la kupambana mambo ambayo yanaweza kuleta madhara katika nchi zote za Jumuiya hiyo na Afrika kwa ujumla.

Alisema yapo madhumuni ya kimkakati,utendaji kivita na kimbinu haya yote yakitekelezwa kwa ufanisi zaidi kwa nchi zote upo uwezekano wa hali ya juu katika mafanikio ya mapambano ya kigaidi na kiharamia.

“Tunajenga misingi mizuri kwa majeshi yetu na kuondoa dhana ya kupambana wenyewe kwa wenyewe sasa tunaelekeza nguvu zetu katika mapamabano ya kigaidi na kiharamia zaidi jambo ambalo litasumbu katika nchi hizi za Afrika”Alisema Meja Jenerali Masebu.

Alisema zoezi hilo litashirikisha Nchi saba za Jumuiya hiyo zikiwa Botswana,Lesotho,Malawi, Jumuiya ya Afrika ya kusini,Zambia, Zimbabwe na Tanzania ambao ndio watakauwa wenyeji katika zoezi hilo ambalo linafanyika hapa kwa mara ya kwanza.

Mkuu wa Mkoa Tanga Martin Shigela aliwaomba wananchi wasiwe na wasiwasi pindi watakapokutana na vikosi hivyo vikiwa vinaendelea na majukumu yao huku akiwataka kutoa ushirikiano pindi watakapo hitajika.

Alisema wananchi wasiokote vitu vyovyote wasivyovielewa na watoe taarifa katika vyombo vya ulinzi na usalama kwa kitu ambacho watakiona kinawapa mashaka.

Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: