Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas kuhusiana na tukio la kuuawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina ya Polisi na wahalifu hao katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Chini ni silaha 8 aina ya SMG pamoja na vifaa vingine zilizopatikana katika majibizano hayo. – Picha na Jeshi La Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha makasha ya risasi (magazine) ambazo ni miongoni mwa makasha 8 yaliyokuwa yakitumiwa na wahalifu katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kushoto ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. Katika tukio hilo Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwaua wahalifu 13 ambao walikuwa wakifanya mauaji Kibiti. – Picha na Jeshi La Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akielezea baadhi ya vitu mbalimbali vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti ambapo jumla ya silaha 8 aina ya SMG, risasi 158, pikipiki 2, pamoja na begi la nguo vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu hao. Kushoto ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya jinai (CP) Robert Boaz
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akionesha silaha aina ya SMG ambayo ni miongoni mwa silaha 8 zilizokuwa zikitumiwa na wahalifu 13 waliouawa katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangibovu, Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti. Wa kwanza kulia ni Kamishina wa Polisi Jamii (CP) Mussa Alli Musa akifuatiwa na Mkuu wa Operesheni Maalumu za Jeshi la Polisi, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Liberatus Sabas. – Picha na Jeshi La Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro akiongea na wananchi wa Kijiji cha Miwaleni Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti alipokuwa akitoka kukagua eneo la tukio walipouawa wahalifu 13 katika majibizano ya risasi baina yao na Jeshi la Polisi katika eneo la Tangibovu. – Picha na Jeshi La Polisi
---
Tarehe 04.08.2017 huko eneo la Gari Bovu, kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Tarafa ya Kibiti, Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Kipolisi Rufiji, Jeshi la Polisi lilimkamata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani akiwa ana majeraha maeneo mbalimbali ya mwili wake akionekana kuwa alikuwa anaendelea kujitibia mwenyewe kwa njia za kificho. Mtuhumiwa huyu, alikamatwa kutokana na kuwepo kwa taarifa za kiintelijensia kuhusu yeye kuhusika na vitendo vya kufadhili, kusaidia, kuhifadhi na kushiriki uhalifu wa ujambazi maeneo mbalimbali. Mtuhumiwa alipohojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili alikubali na alionyesha dhamira ya kwenda kuonyesha Ngome yao.


Tarehe 09.08.2017 majira ya saa 21:00 Hrs (saa tatu usiku) katika mapori ya kijiji cha Rungungu mtuhumiwa akiambatana na Askari Polisi alikwenda kuonyesha Ngome ya watuhumiwa wenzake aliokuwa anashirikiana nao kufanya uhalifu. Baada ya kukaribia eneo la tukio ulitokea upinzani mkali wa majibizano ya risasi jambo lililopelekea hata Abdallah Abdallah Mbindimbi @Abajani kujeruhiwa na risasi sehemu mbalimbali za mwili wake. Kufuatia majibizano hayo, Askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi wahalifu 12 (kumi na mbili. Jitihada zilifanyika kuwapeleka Hospitali majeruhi wote 13 (kumi na tatu) ingawa baadae walifariki dunia kwa nyakati tofauti wakipelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutokana na kuvuja damu nyingi zilizosababishwa na majereha ya risasi sehemu mbalimbali za miili yao. Miili ya marehemu imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es salaam. 

Ndugu Wanahabari

Watuhumiwa 7 (Saba) kati ya 13 (kumi na tatu) waliopoteza maisha kutokana na majibizano ya risasi wametambuliwa kuwa ni:

1. Hassani Ali Njame

2. Abdallah Abdallah Mbindimbi @ Abajani

3. Saidi Abdallah Kilindo 

4. Abdulshakuru Mohamed Ubuguyu

5. Issa Mohamed Mseketu @Mtawa

6. Rajabu Thomas @Roja

7. Mohamed Ally Kadude @Upolo

Miili 6 (sita) iliyobaki haikuweza kutambulika mara moja hivyo utambuzi utaendelea huko ilikohifadhiwa Hospitalini DSM.
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: