Azam TV – Hotuba ya kwanza ya Raismpya TFF Wallace Karia mjini Dodoma

Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF umehitimishwa kwa aliyekuwa makamu wa Rais wa Shirikisho hilo Wallace Karia (kulia) kushinda kwa jumla ya kura 95 na kuwabwaga wapinzani wake.

Uchaguzi huo umefanyika leo mkoani Dodoma ukiwa wa amani kwa wajumbe wa mkutano mkuu pamoja na wagombea wenyewe.

Mwenyekiti wa kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli akitangaza matokeo hayo ambapo alimtangaza Wallace Karia kama mshindi wa kinyang'anyiro kwa kura 95 kati ya kura 127 zilizopigwa.
Wagombea Urais wa TFF na kura zao ni: Emmanuel Kimbe (1). Frederick Mwakalebela (3), Imani Madega (8), Richard Shija (9) Ally Mayai (9) na Wallace Karia (95).

Kuuli ametangaza kuwa, katika nafasi ya makamu wa Rais, Michael Richard Wambura (kushoto) ameshinda nafasi hiyo kwa kura 85.

Kwa upande wa wajumbe wa mkutano mkuu kumekuwa na maingizo mapya kutoka kanda mbalimbali za nchini kama ifuatavyo:

Zone 1: Saloum Chama 
Zone 2: Vedastus Lufano 
Zone 3: Mbasha Matutu 
Zone 4: Sarah Chao 
Zone 5: Issa Bukuku 
Zone 6: Kenneth Pesambili 
Zone 7: Elias Mwanjala 
Zone 8: James Mhagama 
Zone 9: Dunstan Mkundi 
Zone 10: Mohamed Aden 
Zone 11: Francis Ndulane 
Zone 12: Khalid Abdallah 
Zone 13: Lameck Nyambaya
Kajunason Blog

Kajunason Blog

A Tanzanian blog operating since October 2007, covering Local News, Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers / viewers.

Toa Maoni Yako:

0 comments: